Picha za Gari alilopata nalo ajali Sharo Millionair | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
Labels :
Home » » Picha za Gari alilopata nalo ajali Sharo Millionair

Picha za Gari alilopata nalo ajali Sharo Millionair

Written By Mike Ntobi on Friday, November 30, 2012 | 12:52 AM


Hizi ni baadhi ya picha za gari aina ya Harrier T478 BVR alilopatanalo ajali Marehemu Sharo Millionair hadi kupelekea umauti wake. Habari zaidi kuhusu picha za ajali ya gari, pamoja na tukio zima kabla ya ajali, endelea kusoma hapa chini...


Habari za uhakika kuhusiana na chanzo cha kifo cha msanii Hussein Ramadhan a.k.an Sharo milionea ni kwamba gari yake aina ya Toyota harrier ilipata pancha tairi la upande wa kulia na kukosa mwelekeo kisha ikaacha njia na kuelekea mtaroni lakini ule mtalo haukuizuru sana gari hiyo ikaruka na kuingia katika shamba la mahindi.
Kitu kilichoshangaza wengi ni sehemu ambayo si hatarishi sana kiudereva sababu iko tambarare na kona si kali eneo hilo.




Chanzo cha habari kinaendelea kufafanua kuwa baada ya gari kuacha njia ilienda kugonga mti mkubwa na kuung'oa baada ya kuuchana katikati kutokana na gari ilivyokuwa mwendo kasi.

Mwili wa marehemu ulitupwa nje ya gari baada ya kugonga mti huo ambapo gari hiyo iliharibika vibaya kuanzia kwenye roof hadi vioo vyote kupasuka japo vizuizi vilifunguka lakinini havikusaidia.
Kishindo kikubwa cha mlio wa pancha kilisikika kwa wakazi wa kijiji hiko na kuamua kujitokeza kujua nini kimejili pale na wakati wanafika hapakuwa na mwili wa marehemu katika eneo la tukio,ndipo mama mmoja aligundua mwili wa msanii huyo mita chache kutoka gari ilipogonga mti na kuharibika vibaya.

Mganga mkuu wa hospitali teule ya Muheza amesema kuwa chanzo cha kifo cha Sharo ni kubonyea kwa kichwa ikiambatana na majeraha yaliopo kichwani na sehemu ya mabega ndiyo yalipelekea msanii huyo kupoteza maisha papo hapo.

 Hata hivyo jeshi la polisi lilikuja masaa mawili baada ya kutokea ajali hiyo,ambapo gari la Tanesco ndilo lililotumika kuvuta gari hiyo hadi kituo cha polisi wilayani humo. 


Baadhi ya watu wakiliangalia gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.


Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.




Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.



Mbunge wa Jimbo la Muheza Hebert Mtangi akiwasili nje ya jengo la Chumba cha Kuhifadhia Maiti cha Hospitali ya Teule Muheza kwa ajili ya kushuhudia mwili wa msaniii Sharo Millionea aliyekufa katika ajali ya gari wakati akitoka Dar es Salaam kwenda Lusanga, Muheza mkoani Tanga, ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Kijiji cha Songa Kibaoni .


Wakazi wa wilaya ya Muheza na maeneo mengine wakiwa wamefurika nje ya Chumba cha Maiti cha Hospitali Teule Muheza, kusubiri kushuhudia mwili wa Sharo Millionea, aliyefariki kwa ajali ya gari.
Share this article :

Related Posts :

Post a Comment

 
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger