2013 | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
[ New Posts ] : Habari Mpya Zote - HAPA CHINI!!!
Labels :

MGANGA AFUMWA LIVE AKINGONOKA NA MTEJA WAKE ETI NI DAWA...! [Picha]

Written By Mike Ntobi on Sunday, December 22, 2013 | 9:30 AM


Hivi kweli kabisa wewe mwana-dada, umetoka nyumbani kwenu, unafunga safari kwenda kwa mganga wa kienyeji "SANGOMA" ili tu mambo yako yanyooke.... eti unamtaka mme wa mtu, so, inabidi dawa yako dada tuiweke kwa ndani kabisa ya hiyo Libido yako, ukimtaka mwanaume yeyote hakatai.

Sasa maajabu ya mwaka, jinsi ya kuiingiza hiyo dawa huko ndani, ni lazima tutumie hii DUDU yangu , ntapaka dawa hapo kwa mbele halafu ntaingiza dawa taratibu.

Wakati naingiza dawa huko ndani wewe utakuwa unaendelea kukatika kiuno taratibu ukinuia kwamba "MGANGA ONGEZ SPIDI ILI DAWA IINGIE NDANI ZAIDI", Sawa? Binti anajibu sawa mganga nimekuelewa.

JAMANI EEE...! 
NYIE WAGANGA ACHENI KUWALAGHAI WAKINA MAMA HAKUNA DAWA YA KUFANYA NGONO HATA MOJA ACHENI KABISA HUO MCHEZO..!

NA NYIE WAKINAMAMA MNAOPENDA KWENDA KWA WAGANGA EMBU JALINI NA UTU WENU SIO MNAGAWA TU KWA WAGANGA BILA KUPIMA OMBI LA MGANGA, HAKUNA TIBA YA MAPENZI

HEMED Phd AFUNGA NDOA YA SIRI NA BINTI WA KIZAMBIA!!...?!

Hemed na mkewe siku ya ndoa yao huko 
Lusaka, Zambia

               Kuona picha zaidi za yaliyojiri siku wawili hao waliposema 'I DO'.

Video fupi ya tukio hili la kufurahisha itakujia hivi punde endelea kuperuzi blog hii inayokupa habari za kipekee kabisa ambazo huwezi pata sehemu nyingine!!!! 













 Ushahidi wa picha za Hemed Phd akiwa ma mkewe binti wa ki-Zambia Cassie siku ya ndoa yao!!! 

Ooh! Ghosh, kumbe in FILAMU, aaagh!......?

Hii ni filamu mpya kutoka Zambia itakayoitwa Tangled Mess aka Guilt,ni filamu nzuri sana sio ya kukosa.Nitawajulisha mara tu itakapokuwa tayari.

Diamond na Penny Watemana kimapenzi....WEMA SEPETU atajwa kuwa Chanzo Kikubwa..!!

NDIYO habari ya 'mujini' kwa sasa, kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma 'Diamond Platnumz' na mwandani wake, mtangazaji wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mungilwa 'Penny' wamemwagana,  

Penniel Mungilwa 'Penny' na Nasibu Abdul Juma 'Diamond Platnumz'.
KAMA UTANI, WEMA ATAJWA

Kwa sharti la kutotajwa mahali popote, 'mtonyaji' wetu ambaye ni mtu wa karibu wa wawili hao aliliambia gazeti hili kuwa chanzo cha Diamond na Penny kuingia kwenye listi ya 'zilipendwa' kilianza kama utani.
Awali ilidaiwa kuwa kila mmoja amekuwa akijiona mwenye thamani mbele ya mwenzake huku Wema Sepetu naye akidaiwa kuwa chanzo. 

Nasibu Abdul Juma 'Diamond Platnumz' akiwa na Wema Sepetu.


"Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na kila mmoja yuko kivyake.

"Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja anajiona yuko juu kuliko mwenzake, lakini kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na wanawake tofauti mara kwa mara hasa Wema, kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
"Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?" alihoji 'kikulacho' huyo ambaye ni rafiki wa Diamond. 
RISASI MZIGONI
Baada ya kutojiridhisha moja kwa moja na taarifa za awali kutoka kwa rafiki huyo, timu ya gazeti hili kwa kuwatumia 'wahangaikaji' wake maalum, iliingia mzigoni kupeleleza ukweli juu ya tetesi hizo.
Watu kadhaa walio chini ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo rais wake ni Diamond walihojiwa ambapo majibu yalikuwa yaleyale kwamba, kwa sasa Diamond na Penny imebaki stori! 
 SHAKA ILIPOANZIA
Wakati timu yetu ikiendelea na uchunguzi wake makini juu ya uvumi huo, hivi karibuni Diamond alionekana 'singo' kwenye pati ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya 'dada wa mjini', Halima Haroun ' Halima Kimwana' ambayo aliiandaa Diamond.
Minong'ono ya kuhoji kutoonekana kwa Penny ilisikika ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar ilikofanyikia pati hiyo iliyojaa vitendo vya ufuska.

"Haiwezekani leo rais (Diamond) akajiachia peke yake bila Penny. Si kawaida ya Diamond.

"Kwa vyovyote watakuwa wameshamwagana kwa sababu kwenye pati zote huwa wanakuwa pamoja tangu walipoanza uhusiano wa kimapenzi," alisikika mmoja wa waalikwa katika sherehe hiyo.

Katika tukio hilo, Penny alipigiwa simu na paparazi wetu na kujibu kwa kifupi: "Naumwa. Halafu si lazima nije kwani kila mtu ana ratiba zake."

                                                                Penniel Mungilwa 'Penny'.
PENNY KIZIMBANI TENA

Baada ya kukamilisha udadisi huo kupitia kwa watu wao wa karibu, gazeti hili lilianza na Penny kwa kumuuliza undani juu ya habari hiyo lakini alionekana kuwa 'mzito' kwa kutoingia ndani kulizungumzia sakata hilo huku akiahidi kulifungukia muda wowote kuanzia sasa.
"Kwa sasa sina cha kuzungumza juu ya hilo, nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi zijazo, lakini si leo, tafadhali sana," alijibu Penny kwa kifupi na sauti ya chini iliyojaa uchovu.
Paparazi: "Hebu nisaidie, mko wote au hamko wote?"
Penny: "Nimesema sitoweza kusema lolote kwa leo, subirini."

Nasibu Abdul Juma 'Diamond Platnumz'.         

DIAMOND KIMYA
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu yake ya kiganjani, hakupokea licha ya kupigiwa mara kadhaa kwa namba zake zote. Akatumiwa meseji yenye maelezo yote, hakujibu.

MAMA DIAMOND
Ili kujiridhisha na madai hayo, waandishi wetu walimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim 'Sandra' ambaye alisema hajui na hana taarifa hizo.

NDUGU WA KARIBU SANA
Baada ya mama Diamond, paparazi wetu alimpigia simu ndugu wa karibu sana na Diamond, sikiliza:
Paparazi: "Kumbe Diamond na Penny wamemwagana we huniambii. Sasa wifi yako mpya ni nani?"
Ndugu: "Aka! Sikwambii. Kwanza mi nipo mbali, sipo Dar.

WADAU WANAJUA
Haikuishia hapo, timu yetu ilizungumza na wadau mbalimbali ambao walionesha kusikitika huku baadhi yao wakisema walitabiri tangu awali.
"Duh! Penny ameachia ngazi mwenyewe. Sisi tulijua hawawezi kufika mbali, maana penzi lenyewe lilikuwa na mbwembwe nyingi," alisema mwanamke mmoja anayejua kila kitu.

TUJIKUMBUSHE
Siku za hivi karibuni Diamond alifanya mahojiano kwa njia ya mtandao mmoja wa kijamii ambapo moja kati ya maswali aliyoulizwa ni pamoja na mpango wa kuoa ambapo alisema kuwa hana mpango huo kwa sasa na hatarajii kumuoa yeyote kati ya wanawake wanaotajwa kwa sana midomoni mwa watu (akiwemo Penny).
Wema alipigiwa simu juzi, lakini simu yake ilikuwa ikiita 'weee' mpaka inakatika, inaita 'weee' mpaka inakatika.

Mke ampa Kichapo cha Mbwa Mwizi hawara wa Mume wake baada ya Kuwanasa wakila Uroda Gesti - Kinondoni...!!

DUNIA ina mambo jamani! Mfanyabiashara wa madini aliyefahamika kwa jina moja la Jimmy amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufumaniwa na mkewe akiwa na kimada gesti.

Tukio hilo lililofunga mtaa kwa kujaza wambea kibao, lilitokea hivi karibuni ndani ya gesti hiyo (jina tunalo) Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo mke wa mfanyabiashara huyo (jina halikupatikana mara moja), alimnasa mumewe  akijiandaa kuvunja amri ya sita ya Muumba.
Mke wa mfanyaiashara (kulia) baada ya kumfumania kimada akiwa na mumewe gesti maeneo ya Kinondoni, jijini Dar.

Wadakuzi waliokuwa eneo la balaa walitonya kuwa, siku hiyo ya tukio, Jimmy ambaye ni mkazi wa jijini Arusha, alifika Dar kibiashara na baadaye alimsaka kimada huyo wa siku nyingi na kwenda kujirusha naye bila kujua mkewe alishatonywa juu ya usaliti wake.
Awali chanzo makini kinachojua nini maana ya habari kiliwatonya mapaparazi wetu mara baada ya kupata mchongo wa fumanizi kutokea Sinza ya Kumekucha lililoandaliwa na mke wa Jimmy.

"Nyie njooni tu hapa Sinza-Kumekucha ndipo mkewe alipotonywa na dereva wa mumewe kuwa anaibiwa na kimada. Kuna gesti moja ipo ndani kidogo upande wa kushoto kama unaelekea Shekilango," kilisema chanzo.


Timu ya mapaparazi ilifika katika gesti hiyo lakini bahati mbaya  waliambiwa kuwa, Jimmy na kimada huyo walihamisha kiwanja cha starehe na kwenda Kinondoni.


  Kimada aliyefumaniwa na mume wa mtu.
Mapaparazi walipofika katika gesti hiyo ya Kinondoni, walimkuta mke wa Jimmy hivyo wakaambatana naye pamoja na askari polisi wawili kwa ajili ya kwenda kufumania.
Jimmy kabla ya kuingia gesti inadaiwa alijipumzisha katika grosari iliyo karibu na Mango Garden Bar, baadaye akaenda kwenye gesti hiyo ya jirani bila kujua mkewe alikuwa akitua mguu kila pale yeye aliponyanyua, akazama ndani ya gesti hiyo na kuanza kujiandaa kwa zinaa.


Mke wa Jimmy hakuwa mbali, baada ya kujiridhisha mumewe amezama chumbani, dakika kadhaa na yeye alitokea na kugonga mlango wa chumba hicho kufuatia kutonywa na mhudumu mmoja wa gesti hiyo.
Jimmy alikutwa tayari ameshavua nguo zote na kubakiwa na 'boksa' huku kimada naye akiwa na 'kufuli' pekee.

Kilichofuata hapo ni kipigo, mke wa Jimmy alianza kumtembezea kipigo yule kimada. Mapaparazi walivamia na kutandika picha za timbwili ambapo Jimmy alifanikiwa kupenya mlangoni na kukimbia bila kujali nguo nyingine.
Kutokana na kelele za timbwili hilo, majirani wa eneo hilo walifika kuhoji kulikoni ambapo mfumaniaji huyo alitoboa siri kwamba amekuwa akimfuatilia mumewe kwa siku nyingi baada ya kuambiwa ana kimada Dar.


"Huyo malaya akome kutembea na waume za watu. Nimekuwa nikimfuatilia mume wangu kwa muda mrefu. Nimetoka Arusha mpaka Dar kwa ajili yake. Kweli za mwizi ni arobaini, leo nimewanasa," alisema mwanamke huyo huku akiondoka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana.

Wakati pakichimbika, kimada huyo alisikika akimlaumu Jimmy kwamba amemuingiza kwenye mkenge akijua mkewe ni mdodosaji wa mambo na anaweza kufika Dar madai ambayo hayakuwa na wa kuyajibu.
Taarifa zaidi zilidai kuwa ndugu mmoja wa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa na mchoro mzima wa Jimmy na hivyo 'kuuza' kwa mwanamke huyo.

HOTUBA YA MH ZITTO Z. KABWE - KIGOMA – 21 DECEMBER 2013


HOTUBA YA MH ZITTO Z. KABWE - KIGOMA – 21 DESEMBA 2013

Leo nina furaha kubwa sana kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbani kuwasalimu wananchi wenzangu! Na hii si salamu za kawaida bali nawasalimu kwa salaam za demokrasia, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji. Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa Kigoma! Na popote niendapo najivunia kujitambulisha kama Mtanzania; kama mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na zao la Ujiji.
 
Tuna mengi ya kujivunia kama taifa lakini Ujiji na watu wake mna nafasi ya pekee katika historia. Watu wa Ujiji mlipokea harakati za kudai uhuru wa nchi yetu mapema kabisa mapambano ya uhuru yalipoanza. Watu wa Ujiji mlikuwa wa kwanza kabisa kupokea mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Na Jimbo la Kigoma Mjini ilikuwa miongoni mwa majimbo ya mwanzo kabisa kutoa mbunge wa CHADEMA mwaka 1995. Kabla ya hapo mlitoa madiwani wengi mwaka 1994. Wakati Watanzania wengine wakiwa wanajiuliza mara mbili mbili kuhusu kujiunga na vyama vipya vilivyoanzishwa, watu wa Ujiji, watu wa Kigoma hamkusita kupokea mabadiliko. Wengi wamepoteza maisha yao, wengine kazi zao na wengine hata ndoa zao katika kupata
mbegu ya mabadiliko katika nchi yetu. Nawataka msichoke. Wekeni nguvu mpya katika kusimika mabadiliko kwani bado kazi ya kuimarisha demokrasia katika nchi yetu haijaisha na inahitaji uvumilivu, kusameheana na kuaminiana.
 
Na nchi yetu Tanzania ni nchi inayoonyesha uwezo mkubwa katika kupendana, kuaminiana, kuvumiliana na hata kusameheana. Na haya si maneno tu ambayo ninayazungumza kama mwanasiasa. Hii ni hali halisi na maisha niliyoyaishi kwa mifano nilipokuwa ninakua na kusoma katika shule ya Msingi Kigoma na baadaye Shule ya Sekondari Kigoma. Malezi yangu yalikuwa yanaongozwa na jamii nzima ya Kigoma. Nimekuwa nikiwaeleza rafiki zangu niliokutana nao kwenye masomo na kwenye siasa kwamba nimeanza kuvaa viatu kwa mara ya kwanza nikiwa darasa la tatu. Viatu hivyo viliitwa 'asante Salim' vilivyokuwa vinatengenezwa na Kampuni ya Bora Shoes. Vililinunuliwa na mama Coretha Furugunya ambaye tulikuwa tunakaa mtaa mmoja wa Kisangani Mwanga. Mama Coretha hakuninunulia viatu kwa sababu alikuwa ana uwezo mkubwa, la hasha! Alifurahishwa na matokeo yangu ya mitihani ya darasa la pili kwenda la tatu. Ninaamini kitendo cha mama huyu ni ushahidi wa uungwana, upendo na hata uwajibikaji ambao tunao sisi watanzania. Uwajibikaji kwani alichukua jukumu kunilea ingawa hakuwa mzazi wangu, lakini aliona kuwa kama mwanajamii ana nafasi kubwa katika kuwaendeleza watoto wote. Jamii hii ya watu wa Kigoma ilinifunza kuwa nikijitahidi na kukazana kwa bidii kwenye masomo na majukumu, nitafanikiwa. Siwezi kusahau somo hili katika maisha yangu na ni somo hili ndilo limenifanya nijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuwatumikia kwa uadilifu na mafanikio ya hali ya juu sana.
 
Nikiwa nimejaa matumaini haya kuhusu wananchi wenzangu, leo nataka niwakumbushe kwa nini kama jamii tulichagua kufuata njia ya demokrasia. Demokrasia ina maana pale ambapo inatumika kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wananchi. Maisha yanayotakiwa ni yale yanayomwezesha mwananchi kupata huduma zake stahili kama Elimu, Afya, Maji na miundombinu. Demokrasia haina maana pale wananchi wanakufa njaa kwa kukosa ajira na kukuza umasikini. Demokrasia inahusu maendeleo. Tumejitahidi kwa upande wetu kuondoa mkoa wa Kigoma kutoka mikoa isiyo na miundombinu kabisa ya maendeleo mpaka kuwa mkoa unaotumika kama mfano kwa miradi mingi ya Maendeleo ikiwemo Daraja la Malagarasi, Uwanja wa ndege wa Gombe-Mahale, barabara za lami na upanuzi wa Bandari, ujenzi wa bandari ndogo mpya na ujenzi wa kituo cha Usafirishaji Mwandiga. Asije mtu akasema yeye ndio kafanya haya. Haya ni matunda ya nyinyi watu wa Kigoma kupokea demokrasia na bila woga kuchagua viongozi wenu bila kujali vyama bali kwa kuangalia uwezo. Haya ni matunda ya viongozi wenu kupaza sauti yenu kwenye baraza la Taifa, Bunge. Haya ni matunda ya uvumilivu wenu na uamuzi wenu wa kutaka maendeleo. Juhudi hizi lazima ziendelezwe kwa nguvu zote ili kuhakikisha kuwa nafasi ya mkoa wa Kigoma katika uchumi wa Tanzania inaonekana dhahiri na hivyo kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa kituo cha biashara katika nchi za maziwa makuu.
 
Lakini tukumbuke pia kuwa Demokrasia ni Uwajibikaji. Katika kipindi cha utumishi wangu kwenu,kutokana na malezi niliyoyapata kutoka kwenu,nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa Serikali inawajibika kwa Wananchi. Nakumbuka wakati napambana kuhusu sheria mbovu ya madini kuna watu hapa nyumbani walisema 'sasa huyu kawa mbunge wa Taifa' lakini watu wengi zaidi wakasema tumemtuma Dodoma kusemea Watanzania wote na sio Kigoma tu. Tuliweza ndani ya miaka mitano kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye sera ya Madini na sheria ya madini ambapo baadhi ya mambo ambayo yalikuwa hayafikiriki sasa yametungiwa sheria ikiwemo Serikali kuwa na hisa kwenye migodi, Tanzanite kumilikiwa na Watanzania sio chini ya asilimia 50 na kuzuia kabisa wageni kuchimba vito vya thamani. Uwajibikaji ulipelekea kumshinikiza Rais kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri kwa kuwafukuza mawaziri wanane mwaka jana. Hii ilitokana sio tu na hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu bali pia ushiriki mkubwa wa wananchi kupitia simu na mitandao ya kijamii ambapo wabunge walishinikizwa kuweka saini kwenye karatasi za kumtoa Waziri Mkuu. Toka wakati huo kumekuwa na utaratibu sasa ambapo wabunge hawaoni taabu kutaka uwajibikaji waziwazi ili kuzuia ubadhirifu wa fedha za Umma. Ni hivi jana tumeshuhudia mawaziri wanne wamejiuzulu na kufukuzwa kazi kutokana na kashfa ya operesheni Tokomeza ujangili iliyoibuliwa na ripoti ya kamati ya bunge. Mabadiliko haya ni hatua muhimu katika kuimarisha demokrasia yetu.

Pamoja na matunda haya mengi mazuri lakini bado kuna changamoto katika juhudi zetu. 
 
Changamoto kubwa tuliyonayo wananchi ni kukosekana kwa imani katika demokrasia yetu. 

Kutoaminiana. Ni dhahiri kuwa kutoaminiana katika nchi yetu kumekuwa kwa kiasi kikubwa. Taarifa za kitafiti zinaonyesha kuwa katika kila Watanzania kumi, wanane hawaaminiani. Ni changamoto kubwa sana. Wananchi wameacha kutuamini wanasiasa na wanasiasa wameacha kuaminiana wenyewe kwa wenyewe. Hivi sasa uongo umegeuzwa kuwa ukweli na ukweli umekuwa ni uongo. Hivi sasa ukitaka kuwa mwanasiasa maarufu inabidi ujue kudanganya na ukitaka kuitwa mwanasiasa msaliti inabidi uwe msema kweli. Kukosekana kwa uaminifu na kuaminiana imekuwa ni kansa katika siasa zetu. Itachukua muda mrefu sana kujenga demokrasia imara katika nchi yetu kama hatutapata jibu la changamoto hii ya kutoaminiana na kugeuza uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Hivi sasa ukweli umekuwa unatengenezwa badala ya kutafutwa. Ni majanga! Juzi bungeni Mwanasheria Mkuu wa Serikali alielekeza shutuma kwangu kwamba sikushirikiana na kamati maalum iliyoundwa na Bunge kufuatilia mabilioni ya uswisi na kwamba chini ya kiapo nilisema sina majina ya watu wenye akaunti huko Uswisi. Huu ulikuwa ni uongo. Ni uongo kwa sababu niliitika wito wa kamati hata nilipokuwa katika mafunzo ya mgambo huko Tanga na nilikutana nao mara nne. Ni uongo kwa sababu niliwapa wajumbe wa Kamati Maalaum maelezo na taarifa nyingi sana kuhusu utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na umiliki wa mali nje ya nchi kinyumecha sheria. Ni uongo kwa sababu mimi kutotaja majina haya haina maana sina majina, bali ni kwamba ninaheshimu utaratibu na nimeachia vyombo husika vikamilishe uchunguzi. Kwani mimi kama mtu binafsi nikianza kuchukua majukumu ya taasisi ninaweza kutia dosari harakati hizi muhimu na hata kupelekea mchakato mzima kuvurugika. Sitaingia mtego huu! Lakini hatua hii ya Mwanasheria Mkuu imenipelekea kujiuliza maswali mengi kwa mfano uongo kama huu ulifanywa kwa malengo gani? Na ninajikuta hata mimi ninaingia katika hali ninayoilalamikia ya KUTOAMINIANA.  
 
Lakini mtambue pia kuwa kutoaminiana kunaleta kutovumiliana. Hivi sasa kuwa na mawazo tofauti katika vyama vya siasa au hata asasi za kijamii ni uhaini. Lakini bila kuenzi tofauti za mawazo hatuwezi kujenga vyama imara wala Taifa imara. Demokrasia imara ni zao la tofauti za mawazo na uhuru wa mawazo. Kama hatuwezi kujenga vyama vinavyorutubisha uhuru wa mawazo na tofauti za mawazo, tutajenga Taifa lenye watu wenye kuogopa na waliojaa woga. Wanachama wanapoogopa uongozi ni udikteta, lakini uongozi unapoogopa wanachama ni demokrasia. Bila demokrasia ya uwazi na kuvumiliana tutakuwa Taifa la kidikteta. Lazima vyama vya siasa, viongozwe kwa namna ile ile ambayo Taifa litaongozwa. 
 
Demokrasia bila kuaminiana, demokrasia bila kuvumiliana sio demokrasia ya kweli.
Juzi nilipoingia Bungeni kwa mara ya kwanza baada ya matukio kadhaa yanayoendelea ndani ya chama chetu nilikaa pamoja na mbunge Tundu Lissu. Wabunge wengine walidhani tutarushiana ngumi na badala yake ikawa ni vicheko na mazungumzo. Hii ni kwa sababu sina chuki na mtu yeyote yule. Mmenifunza kutojenga chuki na watu na badala yake kuchukua kila tukio kama changamoto ya maisha. Siasa ni kupambanisha mawazo tofauti na hatimaye kutafuta suluhu ya pamoja. Na siasa ina misingi yake ambayo sisi wanasiasa huwa tunasahau kwa maksudi. Msingi wa siasa ni kuwa inapaswa kuleta unafuu wa maisha ya wananchi na sio malumbano tu ya kurushiana maneno na kuzushiana ili kujijengea umaarufu wa kisiasa. Siasa si kuwekeana chuki na kuonyeshana ubabe.

Na hapo ni muhimu muelewa wanaKigoma mnapoambiwa kuwa eti ninapofuatilia mabilioni ya Uswisi ninatafuta umaarufu, ni uongo! Mnaposikia eti kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki na kujitafutia umaarufu, ni uongo! Kinachonisukuma kufanya vyote hivi ni ninyi. Ninasukuwa kila ninapowaona watoto bado wanatembea bila viatu;kila ninapoona akina mama wanapoteza maisha yao katika uzazi;kila ninapoona vijana ambao hawana uhakika wa kupata hata mlo moja kwa siku kwa kukosa kazi; ninapoona wazee wa Kigoma kukosa hata shilingi mia moja kununua chai asubuhi. Ninawaona si wanaKigoma bali mamilioni ya watanzania wakiishi katika hali hii. Alafu nalinganisha na taarifa tunazozipata kuhusu ufujaji na utoroshwaji wa pesa zetu. Hebu sasa linganisheni na ukweli kuwa ripoti ya kimataifa iliyotolewa hivi karibuni imeonyesha kuwa mwaka 2010 pekee, jumla ya dola za kimarekani milioni 1315 (bilioni 1.3), yaani shilingi trilioni  2,113,930,000,000 (sh trilioni 2.1) zilitoroshwa kutoka nchini Tanzania. Mwaka 2011 kiasi cha dola za kimarekani milioni 817 yani shilingi za kitanzania zipatazo trilioni 1,315,370,000,000 (trilioni 1.3) zilitoroshwa. Ripoti hiyo inaeleza kuwa jumla ya fedha za Watanzania zilizotoroshwa nje ya nchi katika miaka kumi iliyopita zilifikia dola za kimarekani milioni 4526 (bilioni 4.5) sawa na shilingi za kitanzania trilioni 7,286,860,000,000 (trilioni 7.3).  Nimewatajia hapa namba chungu nzima na matrilioni na mabilioni hayaleti maana. Lakini hii ina maana kwamba kiasi cha pesa zilizotoroshwa katika miaka 10 pesa - robo yake tuingeweza kujenga barabara ya lami ya kiwango cha juu kabisa kutoka Kigoma mpaka Dar-es-salaam! Pesa hizi zingeweza kuajiri na kuwalipa vizuri walimu, madaktari na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha tunapata huduma bora na kutengeneza ajira bora kwa vijana wetu. Pesa hizi zingeweza kununua madawa muhimu na kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama tunaowapoteza kila mwaka wakati wa uzazi. Pesa hizi zingeweza kuwanunulia watanzania wote si watoto tu angalau pea 10 ya viatu. Sasa nikitafakari haya siwezi kuchapa usingizi mnono na kufumbia macho utoroshwaji wa fedha au matumizi mabaya ya fedha za umma kwa njia ya sisi wabunge kujilipia posho! Hapana! Nafsi yangu hainiruhusu kukaa kimya kwa kuogopa kuitwa mbinafsi au msaliti!
 
Lakini naomba niwasihi kuwa katika nyakati kama hizi za changamoto za kisiasa jambo la msingi kuliko yote ni kutulia maana hakuna linalotokea bila sababu. Licha ya kwamba kuna watu wengi wanapaza sauti zao katika mambo haya lakini pia kuna wengi zaidi ambao wapo kimya lakini wana mawazo yao, ndani na nje ya chama chetu;ndani na nje ya Serikali na ndani nanje ya nchi yetu. Ndio maana lazima kuibadili nchi yetu ili kuweza kuhakikisha kila raia anakuwa na fursa ya kutoa mawazo na fikra zake zinakuwa huru.
 
Maisha ni mabadiliko; mabadiliko hayana ukomo; mabadiliko hayazuiliki kwa sababu bila mabadiliko hakuna ukuaji, bila mabadiliko hakuna maendeleo. Mabadiliko ni kiu kikubwa cha Tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa mpya Tanzania;siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya kweli;siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania. Mungu ibariki Tanzania.

Vitamins & Minerals A-Z: What Do They Do For You?

Vitamin A supports the immune and reproductive systems, bone formation, eyes, hair, skin and teeth. 

You’ve heard of vitamins and minerals, from A-Z, but what are their benefits, and why do you need them? Vitamins are any of a group of organic substances other than proteins, carbohydrates, fats, minerals and organic salts, which are essential for normal growth, development and metabolism of the body. Minerals are just as important for your body to stay healthy. Check out this photo gallery fromBlackDoctor to see how your body uses minerals for everything from building bones to regulating your heartbeat. 

Vitamin B1, or Thiamine, is essential for memory, learning and the normal function of the nervous, muscular and cardiovascular system. 


Vitamin B2 aids in the metabolism of carbs, fats and proteins, and is important in the maintenance of healthy skin, nails and hair growth. 


Vitamin B3 helps support healthy cardiovascular, circulatory and nervous systems, and reduces serum cholesterol. 


Vitamin B5 helps support energy production, cellular building, healing, memory and normal growth. 


Vitamin B6 promotes both mental and physical health, and is involved in more bodily functions that any other nutrient. Its roles include producing antibodies and red blood cells, balancing sodium and potassium and helping to prevent cancer. 


Vitamin B12 is essential for a healthy metabolism, the normal development of red blood cells, a healthy nervous system, and helps all cells function normally.


Vitamin C protects against immune system deficiencies, cardiovascular disease, prenatal health problems, eye disease – and prevents wrinkles


Vitamin D helps to support bones, metabolism, vision, the cardiovascular and nervous system, and helps the body absorb calcium and phosphorus.


Vitamin E helps prevent free radical damage, and is essential for reproduction, cellular health, mental health, healthy blood flow, endurance and healing.


Biotin, a B-complex vitamin, aids in the metabolism of other vitamins, as well as protein, fats and carbs, and supports energy production and healthy hair and skin.


Folic acid is a type of B vitamin that is key for cell growth and metabolism. It is also the standard supplement for pregnant women and women who plan to become pregnant.


Calcium is necessary to build strong bones and teeth in childhood and adolescence. As an adult, you need calcium to maintain bone mass. 


Potassium helps your body maintain a healthy blood pressure.


Magnesium is a nutrient that helps your body produce energy, and helps your muscles, arteries and heart work properly.


Zinc helps the body fight bacteria and viruses, build protein, heal from wounds and supports a healthy pregnancy.


Chromium enhances the action of insulin and appears to be directly involved in carbohydrate, fat, and protein metabolism.

Get our toolbar!Get our toolbar!
  • Alexaporn - XXX (+18) Search!Alexaporn - XXX (+18) Search!
 
Sell Your Products At TripleClicks!Share Links Earn Money!
cafepress.com/nicemike
Sale Online!
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger