![]() |
An Armoured Recoinnaissance VITZ Car, katika maonesho ya gari hiyo England. Hayo ndio maendeleo ya kweli, lakini vile vile ni Burudani pia. |
Yaani hata, ka-NYUMBU ketu ka-long time kugundulika tunashindwa hata kukaendeleza. Tumekalia Majungu, Ufisadi, Uonevu kwa Jamii isiyo na hatia na Unafiki tu. Wenzetu wa majuu (Nchi za Dunia ya 1st) wanaondoka kwa kasi ya ajabu.
Pichani hapo juu, ni gari aina VITZ, lakini imefanyiwa ukarabati na marekebisho hadi kuonekana ilivyo. Ni toleo jipya kabisa la magari ya kisasa, ila mbunifu akaona ni bora ajaribu kuingiza jina lake katika maajabu ya Dunia, na pengine hata kwenye kitabu cha "World Guiness Book" of Inventors.
Je, ni nini sisi kama Watanzania tumefanya na cha Kujivunia? Au hata kwa kupitia migongo ya watu wengine?
Maana hata mbuga za wanyama tunazo za kumwaga tu, cha ajabu Wakenya wanatafuna hela kupitia vivutio vyetu, Wazungu wa majuu ndo usiseme kwani wanajikusanyia mihela kwa kutangaza Rasilimali zetu kuwa ni zao kwani wamesha chukua wanyama wadogo wadogo kibao na kuwapeleka kwao kuwafuga.
Hivi sasa, wana zoo (mbuga) kadhaa zenye wanyama wa kila aina huko kwao, ukiuliza wanyama wamewapata wapi utaambiwa ni hapahapa BONGO COUNTRY.