Pages

Tuesday, September 11, 2012

ALISTAHILI KUUWAWA KINYAMA HIVI? JE..! HII NI HAKI? Ni Polisi-Jamii... AU "Polisi v/s Jamii?!!

RIP - Daudi Mwangosi
Tasnia ya Wanahabari ilimpoteza Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi wa Channel TEN na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Iringa (IPC) katika vurugu zilizotokea kati ya Polisi wa kuzuia vurugu (FFU) na wanachama wa CHADEMA ambapo walikuwa wamekusanyika kwenye ofisi ya chama chao kijijini Nyololo, Mufindi tayari kwa maandamano ambayo yalikuwa yakipingwa vikali na Serikali.