Pages

Sunday, May 04, 2014

Mtoto Anusuru Ndoa ya Bob Junior

Msanii wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’
akiwa na mkewe na mwanaye.
MTOTO wa msanii wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ ametajwa kuwa ndiyo sababu kubwa ya kurejesha ndoa iliyovunjika ya msanii huyo na aliyekuwa mkewe iliyovunjika miezi michache iliyopita.

Msanii wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’.
Akizungumza na mwandishi wetu, msanii huyo alisema kuwa kipindi chote wakati ameachana na mkewe alikuwa akimkumbuka sana mwanaye ambaye alikuwa akiishi na mama yake, Halima.

Raheem Nanji ‘Bob Junior’ akiwa na mwanaye.
“Wakati nimetengana na mke wangu kitu kikubwa nilichokuwa nikikimisi kilikuwa ni uwepo wa mwanangu, nashukuru Mungu kwa sasa nimerudiana naye,” alisema Bob Junior.

No comments:

Post a Comment