HATUFUNDISHWI UKAHABA BONGO MOVIE.....HIYO NI TABIA YA MTU", TUNA-MAKE MONEY.....JACK WA CHUZ | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
Labels :
Home » » HATUFUNDISHWI UKAHABA BONGO MOVIE.....HIYO NI TABIA YA MTU", TUNA-MAKE MONEY.....JACK WA CHUZ

HATUFUNDISHWI UKAHABA BONGO MOVIE.....HIYO NI TABIA YA MTU", TUNA-MAKE MONEY.....JACK WA CHUZ

Written By Mike Ntobi on Saturday, November 17, 2012 | 3:45 AM

JACK WA CHUZ
"BONGO MOVIE HAITUFUNDISHI UKAHABA.....HIYO NI TABIA YA MTU".....JACK WA CHUZ

MSANII wa filamu bongo Jackline Pentzel maarufu ‘Jack wa Chuz’, amefunguka na kueleza kuwa ndani ya tasnia yao hakuna mwanamke changudoa au muhuni na kama yupo basi huyo alikuwa na tabia hiyo hata kabla hajaingia katika fani hiyo.

Kauli ya msanii huyo inaweza kuwa na ukweli ndani yake kwani wasanii wengi wametoka sehemu mbalimbali ndani ya taifa hili, hivyo inawezekana uchangudoa alikuwa nao kitambo lakini hakuna anayefundishwa tabia hiyo akiingia bongo movie.
 


JACK WA CHUZ
Msanii huyo alisema kuwa wasanii wote ni watu wazima na wana akili zao timamu hivyo wanaopenda kuitwa wahuni au changudoa basi hao watakuwa na kasoro kwani wapo baadhi hawafanyi filamu ili kujiuza kama watu wanavyodai na kikubwa ni kuelimisha hasa kwa wale wanaopenda kutazama kazi zao.
 

“Hakuna msanii wa kike anayefundishwa ukahaba ndani ya bongo movie na kama yupo aliyewahi kufundishwa basi awataje waliomfundisha, nachoelewa mimi ni kwamba kama yupo msanii wa kike changudoa basi tabia hiyo alianza hata kabla hajaigia kufanya filamu,”
 alisema.

Jack alidai kuwa zipo taarifa kadhaa ambazo zimekuwa zikidai kuwa baadhi ya wasanii wa bongo movie ni machangudoa lakini ishu hizo huwa zinawagusa wote, wakati wahusika wakuu wa tabia hizo ni wale ambao wametoka kwenye mashindano fulani ya urembo.

Kama ni mpenzi  wa kucheki filamu za Kibongo, haina shaka utakuwa unaifahamu orodha ndefu ya mastaa wa kike wanaofanya vizuri kwenye tasnia  hiyo.

Kwenye exclusive interview aliyofanya na mtandao huu mwishoni mwa wiki iliyopita staa wa Jumba la Dhahabu, Jaclyn Pentezel ‘Jack wa Chuzi’, amefunguka kuwa sasa anajihisi milionea kufutia mshiko havi anaingiza kwa mwaka kupitia  uigizaji.


Jack Wa Chuzi ‘super star’ wa muvi asiyekaukiwa matukio ameiarifu mpekuzi  kuwa sasa anauhakika wa kuingiza kiasi cha shilingi za kibongo milioni 18 kwa mwezi  kupitia malipo ya shilingi milioni 6 kwa kila muvi anayoigiza.

“Kwa sasa mtu akija na kazi yake sichezi chini ya shilingi milioni 6, ni kiwango ambacho ninaamini kiko kwenye hadhi yangu, ninafuraha kwa sababu sasa najihisi milionea” alisema Jack wa Chuz.

Akiendelea zaidi Jack alisema kuwa sasa anauhakika wa kumiliki milioni 360 kwa mwaka endapo ratiba yake ya kucheza muvi 3 kwa mwezi haitabadilika.
Huo ndiyo umilionea wa Jack wa Chuzi.
Share this article :

Related Posts :

+ Comments: + 2 Comments:

2:08 AM, November 20, 2012

Money by all means!

Anonymous
5:53 AM, November 24, 2012

Thanks for your marvelous posting! I actually enjoyed
reading it, you are a great author.I will make sure to bookmark your blog and will often come back in the future.
I want to encourage yourself to continue your great writing, have a nice morning!
Here is my web site - Spray For Premature Ejaculation

Post a Comment

 
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger