MIKENTOBI: Politics | A Blog with updated posts about events and current issues! MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
[ New Posts ] : Habari Mpya Zote - HAPA CHINI!!!
Labels :
Showing posts with label Politics. Show all posts
Showing posts with label Politics. Show all posts

Obama, Pope Francis meet for first time

Written By Mike Ntobi on Thursday, March 27, 2014 | 9:17 PM

Watch this video


Watch this video

President Obama meets the Pope



STORY HIGHLIGHTS
  • The meeting between the Pope and the President could help smooth tensions with Catholics
  • Abortion and Obamacare mandates on contraception are areas of disagreement
  • One place for common ground could be the plight of immigrants and the poor
  • Pope Francis' popularity could give President Obama a small bump in the polls


(CNN) -- President Barack Obama gave Pope Francis a bag of seeds as a gift, a fitting token as their first-ever meeting provided a fresh start of sorts between the administration and Catholic leadership after years of strained relations.
"These, I think, are carrots," Obama told the Pontiff, showing him one pouch. The seeds were inside a box made from timber from the first cathedral to open in the United States, in Baltimore.
The two world leaders greeted each other with a smile and a handshake, and posed for pictures before sitting down across a table from each other.
It was an important meeting that had its share of light moments.

Photos: Popes and U.S. presidents
Photos: Popes and U.S. presidents

Pope Francis\' first year
Pope Francis' first year


Rock star Pope shakes up the Vatican
The President at one point quipped, "His Holiness is probably the only person in the world who has to put up with more protocol."
The goal of the meeting: Focus on areas where two of the world's most influential men agree and gently tread ground where they differ.
In an interview with the Italian newspaper Corriere della Sera, Obama pointed to the Pope's concern for income inequality, saying, "Given his great moral authority, when the Pope speaks it carries enormous weight."
Continuing to focus on income inequality, Obama said, "And it isn't just an economic issue, it's a moral issue. I think the Pope was speaking to the danger that over time we grow accustomed to this kind of inequality and accept it as normal. But we can't."
The President said he admires the Pope's courage to speak out on economic and social issues.
"It doesn't mean we agree on every issue, but his voice is one that I think the world needs to hear. He challenges us," Obama told the newspaper. "He implores us to remember the people, especially the poor, who are affected by the economic decisions we make."
The meeting took place two days after the U.S. Supreme Court heard arguments on a contraception mandate included in the President's signature health care reform law.
The law exempts churches and houses of worship from the requirement, but nonprofit, religiously affiliated groups are required either to provide contraception coverage to their employees directly or through a third-party insurer.
The U.S. Conference of Catholic Bishops has been vocal in its opposition to the provision, said Sister Mary Ann Walsh, a spokeswoman for the organization.


Pope Francis' most irresistible moments


Jimmy Carter for Catholic women priests

Photos: Gateway for migrants, refugees
Photos: Gateway for migrants, refugees
"Religious liberties and right-to-life issues are a concern," she said of the tension between American Catholic leadership and the administration. However, "the U.S. bishops have appreciated the administration's cooperation on issues of mutual concern."
Those areas of "mutual concern" include immigration and poverty -- issues where the President and the Pope could find common ground.
Francis underscored his commitment to the plight of immigrants during a trip last year to the Italian island of Lampedusa, a place where thousands of African migrants desperately fleeing political upheaval and poverty pour onto European shores. Many die in the attempt to cross.
Next month, a group of American Catholic leaders, including Cardinal Sean O'Malley, the archbishop of Boston, will follow suit and travel to the U.S.-Mexico border to highlight immigration concerns.
On Wednesday, the administration renewed its public call for immigration reform by backing an effort by House Democrats to force a vote on the matter.
"Immigration reform is the right thing to do for our economy, our security, and our future," the White House said in a statement.
Tensions between the administration and many leaders in the American Catholic community began early in the President's tenure over his support for abortion rights.
A number of bishops criticized the University of Notre Dame's decision in 2009 to award Obama an honorary law degree and invite him to give the commencement address.
Relations frayed further over the contraception coverage requirement in Obamacare, leading the U.S. Conference of Catholic Bishops to pan the law.
"It was a very tough year," said Christopher Hale, a senior fellow with Catholics in Alliance for the Common Good who helped lead national Catholic outreach for Obama's 2012 re-election campaign. "It was hard to find any reasonable Catholic who thought the Health and Human Services mandate was handled well."
Differences over same sex-marriage only added to the strained relationship.
Religious experts said Francis would not have been likely to wade into politically charged conversations during the meeting.
"The Vatican has to be very careful to not create a gap between what they're saying and the bishops are saying," Schneck said. "They will be very careful not to undercut the American bishops in that regard."
The meeting with Francis, whose approval ratings are in the high 80s, might also boost Obama in that regard. His standing with the public has hovered in the low 40s.
After all, the Pope's name and quotes have been invoked in everything from discussions over unemployment insurance, the minimum wage and the bigger issue of income inequality.
"If I was advising President Obama, I would say the No. 1 spokesperson on American immigration reform should be Pope Francis," Hale said. "He has so much capital in this city. You have Catholics, Jews and atheists on the Hill quoting him."
House Speaker John Boehner, an Ohio Republican and a Catholic, recently invited the Pope to address a joint session of Congress.
"Everybody on the planet would like to have their picture taken with the Pope these days," Schneck said. "One of the things that would delight Obama is if some of that popularity would rub off. Given the President's current low numbers, he is hoping for a bit of a boost."
CNN's Ed Payne contributed to this report.

Ukarabati wa Jengo la Bunge: Shilingi 8,200,000,000/= zadaiwa kutumika..!!??##$$

Written By Mike Ntobi on Wednesday, February 19, 2014 | 1:15 PM

Ukarabati wa Jengo la Bunge: Shilingi 8,200,000,000/= zadaiwa kutumika!

- Wadau wadai ni vigumu kuamini hizo pesa zimetumika, na kusema zingeweza kujenga Jengo jipya la Bunge lingine jipya. Waitaka Serikali kutoa Maelezo ya Kina!

Una maoni gani? Zaidi fuatilia => http://bit.ly/1gDskkk

MALUMBANO JF YAMTOKEA PUANI MTOTO WA KIGOGO WA SISIEM AISHIE NJE YA NCHI.

Kama mwananchi wa Tanzania, nimeshitushwa sana na habari za pesa zilizotumika kukarabati Bunge kwa ajili ya Bunge la Katiba, siamini kwamba hizo pesa ni kweli zimetumika kukarabati tu.

Kwa maoni yangu, hizo pesa kama kweli zimetumika basi zingeweza kujenga jengo jingine jipya kabisa la bunge pembeni na bunge la sasa unless kuna something I am missing on the issue. 
...Nilishtuka sana baada ya kusoma hio figure. Na bado watalipwa 300,000 kila siku kwa kukalia hivo viti:


Wadau wadai ni vigumu kuamini hizo pesa zimetumika, na kusema zingeweza kujenga Jengo jipya la Bunge lingine jipya. Waitaka Serikali kutoa maelezo ya kina.

ENZI HIZI HAPA CHINI, HAYO MAUJINGA YASINGETOKEA HATA KIDOGO:

Filipo's Avatar

Mimi nadhani hizo pesa ni nyingi mno, zinahitaji kutolewa maelezo na wahusika au kama humu ndani kuna wasomi wa ujenzi wanipe darasa kidogo, kwani siamini kama ni kweli tumekarabati tu bunge kwa Billioni 8.2! 

Mabishano kadhaa NDANI YA JF: 

"Umesahau ripoti za CAG juu ya ubadhirifu, hatua gani zimechukuliwa kwa wahusika?
Kama chama kingekuwa makini huo ujasiri wa kutumia 8.2bilion kukarabati ukumbi ungetoka wapi? Ndo maana nakuambia subiri vikao vya ndani maana kwenu ni biashara kama kawaida'.
Sana sana huwa tunaona wanaolalamika toka huko ni wale waliokosa 'mgao' siyo kuwa na uchungu na rasilimali zetu!". 

"Kaka hapa ninaongea Taifa sio chama, hizo pesa ni nyingi sana mkuu wangu kwa ukarabati tu na it does not make any sense at all!!"

"Unanafasi ya kumuuliza mwenyekiti wako wa ..., Mama M......, au N.... akusaidie kuuliza... ww ndo unashangazwa na ubadhilifu huu??? Kama ni Taifa linaloongea, CHADEMA unayo kadi, CUF unayo kadi, NCCR unayo kadi. Acha kutuzingua na wewe, kama Baba yako hakukuandaa ule umeshachelewa. Endeleza utapeli nja misifa tu huko Nigeria kwa matapeli wenzio. Watanzania, tumechoshwa na kusikia majina yaleyale tu kila siku" 

"Hivyo ndivyo mlivyo,nashangaa leo unawashangaa wenzako!!!!au hukupata mgao? Ufisadi sio tatizo hapa Tanzania bali ni sera ya chama chenu." 

"Leo ndo umeshituka mbona kuna pesa nyingi tu zinatumika ndivyo sivyo au hizi unadai kwa vile Sio mmoja wa washikaji walioteuliwa?" 

"Upo ukumbi mpya kabisa wa Mwalimu Nyerere umejengwa na Wachina Dar ambapo wengi wa wajumbe wanaishi. Kwanini hatukuukodi huu kuendeshea vikao vya bunge? Labda serikali ingesevu gharama za nauli, mafuta ya wabunge kwenda Dom. Sasa, Mafuta wanapewa kwenda Dom, Bil 8.2 zimeyeyuka, matatizo yako palepale, vifo vya kukosa dawa, watoto hawana madawati na vitabu mashuleni, kodi zinazidi kupandishwa tu hadi "LINE ZA SIMU TULIPIE KODI" Watanzania kila fursa inageuzwa kuwa deal/ulaji hadi misiba!" 

"Kaka ni kutumia akili japo kidogo tu then utajua kwamba hizo zilizotumika ni pesa zilizoidhinishwa na Bunge wakiwemo WapinzanI"

"Kaka sihitaji kuteuliwa kwenye anything ndio maana nipo huku Lagos nafanya mambo yangu, pole sana mnaishi kwa kusubiri kuteuliwa, pole sana kaka!!" 

"Inavyoelekea unataka tukunyang'anye kadi ya chama. Unasema unaongea taifa, kwani chama tawala ni cha taifa gani? Kwa nini huulizi maswali ya namna hii kwenye vikao vya ndani? Au na wewe unataka sifa? Au kwa kuwa haujateuliwa bunge la katiba kupitia watu wenye malengo yanayofanana? Usituharibie taswira ya chama, una fursa nyingi tu za kupata ufafanuzi wa fedha hizo, lakini kwa makusudi tu umekuja kuiweka huku JF. Tuheshimiane tafadhali!" 

"Kaka sihitaji kuteuliwa kwenye anything ndio maana nipo huku Lagos nafanya mambo yangu, pole sana mnaishi kwa kusubiri kuteuliwa, pole sana kaka!!"

"Hapo kwenye red + Avator yako ni dalili tosha za mwanaume kutojiamini." 

"Any way, mada yako ya leo ina mashiko lakini hata hivyo ni unafiki tu kwa sababu serikali ya chama chako imefanya madudu makubwa mno zaidi ya haya na siku zote mnafumbia macho. Naungana na mchangiaji aliyesema unalalamika kwa sababu hukuchaguliwa." 

"Mzee wa babes achana hawa jamaa ni wivu wa kike tu! Is unajua wewe ni mtu wa kupiga kazi sana? Hawajui hilo na sasa hivi uko zako hivyo, na umeingia kupiga kazi toka saa nane usiku au siyo?
Eeb bana pamoko sana wasalimie ma-babes wa huko bana ukijimwaga. Club baadae...
Ungepiga kazi tu mtu wangu, maana si- unavyeo vya kutosha tu kuulizia haya maubadhilifu. Ndani ya vikao halali...ebu nikumbushe? Kuna mjumbe sijui, halafu mlezi...halafu nini tena vile.."

"Le Mutuzi unajiandaa kwa ajili ya jimbo la mtera...utapita kwa Nabii TB Joshua ukiwa Hapo Lagos....?" 

"Le mutuz Leo hauko upande wao kuwatetea? Au machungu ya kutokuchaguliwa kuingia mjengoni. 
Kwanza hongera kwa kusemea hilo, ni Kweli kabisa umesema. Ni dawa kiasi gani kwenye zahanati na vituo vya afya zingepelekwa? Madawati mangapi yangenunuliwa? BRN wanafunzi wanakaa chini? Aibu yetu Tanzania na serikali."

Wafuasi wa CHADEMA waandamana wakimshinikiza Godbless Lema ajiuzulu kwa kuwa jimbo limemshinda

Written By Mike Ntobi on Monday, January 27, 2014 | 11:42 AM


Wafuasi wa CHADEMA jijini Arusha walioambatana na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli Bw. Amani Salenga wakionyesha bango hilo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)..

Amani Salenga akiwa na kundi kubwa la vijana walikutana na waandishi wa habari na kudai kuwa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema ndo chanzo cha vurugu ndani ya CHADEMA kwa kuanzisha kikundi cha vijana kinachohatarisha maisha ya wale wanaopinga na mawazo ya Lema katika utendaji wa chama mkoani Arusha.
 
Amani alisisitiza kuwa kwa kuwa CHADEMA  imeamua kufanya maamuzi kwa maslahi ya watu binafsi hususani swala la viongozi waliovuuliwa vyeo vyao(zitto),basi kila mwanachadema  anatakiwa atambue kuwa ndani ya chama hicho kuna pande mbili , CHADEMA ASILI na CHADEMA FAMILY.


Vijana hao waliokuwa na mabango mbalimbali wamelaani  hatua  ya  chama  chao  kuwafukuza  viongozi  wao  pasipokufuata  katiba  ya  chama  na kusisitiza kuwa Lema ndo tatizo ndani ya Chadema.

JK amuweka kitanzini Profesa Kapuya


RAIS Jakaya Kikwete ameviagiza vyombo vya dola kuhakikisha vinamkamata mtu yeyote bila kujali cheo, atakayebainika kumbaka au kumuoa mwanafunzi wa shule. 
Ametoa kauli hiyo huku aliyekuwa waziri wa wizara tofauti katika awamu mbalimbali za uongozi, Profesa Juma Kapuya, akiandamwa na tuhuma za kumbaka na kutishia kumuua binti, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.
Ingawa Rais Kikwete hakutaja jina, lakini ni dhahiri kuwa kauli hiyo inamgusa pia Profesa Kapuya, Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM).
Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara kwenye wilaya za Itilima, Meatu na Maswa mkoani Simiyu, Rais Kikwete alisema mtu anayefanya mapenzi na wanafunzi lazima akamatwe, ahojiwe na kufunguliwa mashitaka ya ubakaji na si vinginevyo.
"Kuna watu wanafanya mapenzi hadi na wanafunzi wakati sote tunajua ukimwi upo na hauna dawa na unaua. Kwa hiyo kila mmoja wetu awe makini kujikinga nao na tuepuke kuwaambukiza wengine," alisisitiza Rais Kikwete.
Wakati Rais Kikwete akisisitiza wahalifu wa makosa ya kubaka na kuoa wanafunzi wachukuliwe hatua, polisi jijini Dar es Salaam wamekuwa wakisuasua kumchukulia hatua Profesa Kapuya licha ya binti anayedaiwa kumbaka, kufungua jalada namba OB/RB/21124/13 katika kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, akidai kutishiwa kuuawa na mbunge huyo.
Kauli ya Rais Kikwete imeonyesha dhahiri kukerwa na moja ya ujumbe mfupi wa maneno wa simu ya mkononi kutoka kwenye simu inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya kwenda kwa binti aliyebakwa, ambapo mbunge huyo alijigamba kwamba serikali haiwezi kumfanya chochote.
Ujumbe huo unasomeka hivi: "Mkiuawa itakuwa vizuri…itawapunguzia gharama za kuishi, usitake kugombana na serikali mtoto mdogo kama wewe, sisi ndiyo wenye nchi yetu, mwenye hilo gazeti ni Mbowe, sasa mwambieni nyumba ya kuishi si mmemuingizia hela leo?
 Mnatumika tu bure watu wanaingiza hela nyingi, ila mmenitibua lazima niwaue, wiki hii haitaisha, nitapiga kambi kote, jana si wamekuficha, tuone utalindwa milele, maana washatengeneza hela, lazima mvae sanda tu, hilo sio ombi ni wajibu wenu, mnajitia na nyie mafia watoto siyo, watoto wetu wanauza unga nani anawakamata? Nani atapingana  nasi."
Habari kutoka Ikulu ya Rais Kikwete zinaeleza kuwa kiongozi huyo wa nchi amekerwa na kauli ya mbunge huyo wa Urambo Magharibi kwamba serikali haiwezi kumfanya jambo lolote.
Ni kutokana na kauli hiyo, mtoa taarifa wetu alisema rais aliagiza vyombo vya dola kufuatilia kwa karibu sakata hilo na kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake.
Pamoja na msimamo wa Rais Kikwete na binti anayedaiwa kubakwa kuripoti polisi, Profesa Kapuya alifanikiwa kusafiri nje ya nchi huku polisi wakimshuhudia bila kumtia mbaroni.
Akiwa nje ya nchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikaririwa mara kadhaa akijigamba kuwa polisi inamsaka mbunge huyo na itamtia mbaroni mahala popote alipo.
Hata hivyo, Profesa Kapuya alirejea nchini juzi huku polisi wakimshuhudia bila kuchufkua hatua zozote.
Mwanafunzi huyo anadai kubakwa na Profesa Kapuya kwenye moja ya hoteli ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho ndani ya ofisi yake katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipomuita kwenda kuchukua ada.

Taarifa ya CHADEMA: Ufafanuzi kuhusu tamko la Ndugu A.O. Chitanda



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU A.O. CHITANDA


Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu A.O. Chitanda, huku pia waandishi wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;

Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama, Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, mjadala wake kwa upande wa chama umeshafungwa, huku taratibu za kikatiba za ndani ya chama zikiendelea.

Pili suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni 
wapya;
  1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
  2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).
  3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
  4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
  5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.


Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.

Kama ni suala la kuangalia mtu anatokea wapi (ambalo halijawahi wala haliwezi kuwa moja ya vigezo), ili kuonesha ukweli na kubainisha uongo wa watu wanaojaribu kufanya kazi ya CCM wakisema wao ni wanCHADEMA, kwa kutumia propaganda zile zile na kuzifanya kuwa ni kete zao za kisiasa, tunaweza kutaja maeneo ya wanakotoka au asili yao kama ifuatavyo;

  • Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji, Antony Komu- Kilimanjaro.
  • Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare- Kagera.
  • Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila- Dodoma.
  • Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John John Mnyika- Mwanza
  • Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema- Kilimanjaro.
  • Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala- Morogoro.


Hadi sasa uteuzi wa kurugenzi za Makao Makuu ya CHADEMA haujakamilika. Bado kuna nafasi zinazotakiwa kujazwa kwa kufuata taratibu za chama.

Hii ni kwa sababu restructuring, inayofanyika ndani ya chama, hadi sasa inaendelea katika ngazi ya Makao Makuu na kanda, kisha itaendelea kwa ngazi za mikoa, wilaya, majimbo, kata, kijiji na hatimaye kitongoji.

Katika restructuring hiyo ya nafasi za uteuzi, inayoendelea sasa ambayo inakwenda hatua kwa hatua, hadi kuwa na makatibu wa kuajiriwa ngazi ya chini ya chama, chama kinazingatia uwezo, uadilifu na utayari wa mtu katika kutoa utumishi bora kwa wanaCHADEMA na Watanzania wote katika nafasi husika.

Suala la maslahi ya watumishi wa CHADEMA ni utaratibu wa chama ambao unajadiliwa, kufikiwa uamuzi na kisha kuridhiwa kwenye vikao vya chama, kama ilivyofanyika kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichoketi karibuni.

Katika suala hili la maslahi ya watumishi wanaojitolea Makao Makuu ya CHADEMA ambayo si siri, Ndugu Chitanda amesema uongo mkubwa. Kwanza si kweli kuwa Ofisa Mwandamizi anaweza kulipwa posho kubwa kuliko Mkurugenzi wa kurugenzi husika.

Ndugu huyo anadhihirisha uongo huo yeye mwenyewe kwa kuandika hivi; "800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanzia Tshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs. 6,800,000/= kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni Tshs. 1,000,000-1,500,000/=".

Pia si kweli kuwa kila mtumishi anayejitolea Makao Makuu analipwa. Mathalani, wakurugenzi wenye nafasi za ubunge, hawalipwi hata shilingi moja kwa kazi zote wanazokitumikia chama na Watanzania kwa ujumla.

Kwa maelezo hayo ya kutengeneza, ni kwamba hadi sasa Ofisa Mwandamizi anapokea posho kubwa kuliko Mkurugenzi na hata baada ya 'restructuring' atapata posho kulingana na Mkurugenzi. Anapaswa kuwa mkweli. Mtu anayetaka kuonekana muungwana, anapaswa kujiweka mbali na uongo pamoja, maneno ya kutunga pamoja na upotoshaji wa makusudi.

Kama ilivyoandikwa hapo juu, *restructuring* inaendelea. Ni hatua kwa hatua. Itafika ngazi za chini kama Baraza Kuu lilivyoagiza. Kwa sababu hiyo hadi sasa uteuzi wa Makatibu wa Mikoa na Wilaya haujafanyika.

Hata hivyo ruzuku imekuwa ikipelekwa kila kanda, mkoa, wilaya na jimbo kama ilivyoridhiwa na Kamati Kuu. Na hii ni zaidi ya pikipiki, kompyuta na magari yaliyopelekwa kila kanda. Angelikuwa mkweli, nagelisema na hili pia.

Ndugu Chitanda anajichanganya katika taarifa yake yote. Hii ni moja ya sifa ya kukosa hoja hivyo mtu anaamua kuibua viroja au kutunga maneno kwa sababu ya kushindwa kusema ukweli.

Anaonesha kuwa alikuwa mtu aliyeaminiwa hadi kuwa katika vikao muhimu, lakini wakati huo huo anasema kuna ubaguzi! Tunapaswa kumhurumia kwa kushindwa kuunganisha hata mawazo yake na kupata mtiririko wa hoja zenye mantiki! Angelikuwa mkweli angesema katika vikao vya sekretarieti na CC, aliingiaje kama kuna ubaguzi wa dini!

Kwa sababu anazozijua yeye, Ndugu Chitanda ameamua kujipachika cheo ambacho hajawahi kuwa nacho. Amejiita kuwa ni Katibu wa Sekretarieti ya Makao Makuu.

Ndani ya CHADEMA pamoja na kwamba nafasi hiyo imetajwa ndani ya Katiba ya Chama, hakuna mtu ambaye ameteuliwa kutumikia nafasi hiyo. Kama anaweza athibitishe kwa kutoa barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu Mkuu.

Mahali pengine amejitambulisha kuwa ni Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu. Ofisi hiyo ina Katibu Mtendaji mmoja ambaye ni Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa CHADEMA.

Operesheni ya Chama inayoendelea nchi nzima kwenye majimbo 103, si suala la siri wala lengo bovu kama anavyotaka umma uamini.

Ni mwendelezo wa mpango mkakati wa chama kupitia progamu za Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), unaotekelezwa kwa hatua mbalimbali na kwa mbinu tofauti tofauti pamoja na dhana ya CHADEMA ni msingi.

Operesheni hiyo ambayo ni mwendelezo wa nyingi za namna hiyo zinazokwenda ngazi za chini kabisa za chama, zikilenga kuimarisha taasisi na mifumo, imeanza wiki hii na ilitangazwa mbele ya waandishi wa habari.

Tungependa kumalizia ufafanuzi huu mfupi kwa kutoa tahadhari kwa umma kuwa makini na matamko ya watu wa namna hii. Maana tunajua kwa uhakika yako mengi ya namna hii yatatokea kadri ambavyo Watanzania wanakaribia kuona na kuishi matumaini ya mabadiliko ya kiutawala na mfumo ndani ya nchi yao.

Mathalani katika taarifa yake, Ndugu Chitanda amedhihirisha na kuonesha kuwa ni aina ya watu ambao wanaCHADEMA na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuwaangalia kwa macho ya kuhoji na tahadhari ya hali ya juu, anasema hivi;

"Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda."

Aya hiyo pekee inayotumia lugha wanayotumia mahasimu wa CHADEMA, wakiongozwa na viongozi waaandamizi wa CCM, wanaohangaika kutokana na Watanzania kuwakataa, wakijiandaa kuwaondoa madarakani kwa sababu sera zao zimeshindwa, inatosha kuonesha uhalisia wa taarifa yake yote.

Ni kauli za namna hii (kuwatisha na kutaka kuwatenganisha Watanzania) ambazo zimekuwa zikitumiwa na watawala kama njia pekee ya kutaka kuzuia upepo wa mabadiliko unaovuma nchi nzima, zimekuwa zikiwaunganisha zaidi Watanzania kuiunga mkono CHADEMA bega kwa bega, ili kupata haki na matumaini ya wanyonge, katika mapambano ya awamu ya pili, kuelekea uhuru wa kweli.

Imetolewa leo Novemba 30, 2013, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA

Marais wa Eac watia saini huko KAMAPALA kuhusu itifaki ya kutumia sarafu moja..!!

http://www.wavuti.com/uploads/3/0/7/6/3076464/5763105_orig.jpg

L-R ni Marais: Pierre Nkurunzinza (Burundi), Jakaya Mrisho Kikwete (Tanzania), Uhuru Kenyatta (Kenya), Yoweri Museveni (Uganda) na Paul Kagame (Rwanda) muda mfupi baada ya kutia saini itifaki ya Umoja wa Fedha wa Afrika Mashariki (picha: Freddy Maro/IKULU)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo kwa pamoja wametia  saini itifaki ya Umoja wa Fedha  wa Afrika Mashariki, (The East African Monetary Union) katika hoteli ya Speke, Munyonyo  mjini Kampala.

Marais waliotia saini itifaki kwa niaba ya wananchi wao ni Jakaya  Mrisho Kikwete wa Tanzania, Pierre Nkurunziza wa Burundi, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda .

Mara baada ya utiwaji wa saini, itifaki ya Umoja wa Fedha itapelekwa Kwenye mabunge ya nchi wanachama kwa ajili ya 

kuridhia ifikapo Mwezi Julai mwaka 2014.

Utiaji wa saini huu unaanzisha mchakato wa kuelekea kuwa na sarafu moja ifikapo mwaka 2024 kwa nchi za Afrika Mashariki.

Kikao cha viongozi pia kilishuhudia Rais Kenyatta akichukua Uenyekiti wa Jumuiya kutoka kwa Rais Museveni na kuelezea matarajio yake ya Jumuiya  kukua zaidi na kuzitaka nchi wanachama kuelimisha zaidi wananchi wa Afrika Mashariki kuhusu faida za Ushirikiano huu.

Itifaki ya Umoja wa Fedha ni ya tatu baada ya itifaki ya Umoja wa Ushuru wa Forodha na itifaki ya soko la pamoja na hatimaye kuelekea kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki.

Katika mkutano wa Leo, mbele ya viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mwanafunzi Peter Robert kutoka shule ya sekondari Tushikamane, Morogoro amepokea cheti na zawadi ya fedha taslimu baada ya kuibuka mshindi wa shindano la kuandika Insha inayohusu EAC.

Mara baada ya kikao,,Rais Kikwete amerejea jijini Mwanza kuendeleza na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Simiyu ambapo kesho tarehe 1, ataendelea na ziara katika Wilaya ya Busega.

Mwisho.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Kampala, Uganda
30 Nov 2013

CHADEMA yazidi kupukutika...Mwekiti wa chama Mkoani Lindi nae Ajiengua, Anena Siri Nzito kuhusu Chama hicho..!!



SASA ni dhahiri kwamba hali si shwari ndani ya Chadema, baada ya viongozi zaidi kuendelea kuachia ngazi kwa kile walichodai kuchoshwa na hali ya mambo katika chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Said Arfi kujiuzulu wadhifa wake mwishoni mwa wiki iliyopita, jana ilikuwa zamu ya Mwenyekiti wa Chadema mkoani Lindi, Ally Chitanda aliyetangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya chama na pia kujivua uanachama.
Mbali ya kuwa Mwenyekiti wa Mkoa, kabla ya uamuzi wake huo uliotangazwa jana, Chitanda pia alikuwa Katibu wa Sekretarieti katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema Taifa katika makao yake makuu yaliyopo Mtaa wa Togo, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Alikuwa pia Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.
Chitanda alianika uamuzi wake huo jana katika mkutano wake na wanahabari mjini Lindi, akisema amechoshwa na unafiki na uonevu unaoendelea ndani ya chama hicho alichojiunga nacho miaka kumi iliyopita akitokea NCCR-Mageuzi.

Alisema kikao cha Kamati Kuu kilichoketi kwa siku mbili na kufikia maazimio kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwavua madaraka Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto, Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ndiyo yaliyomchefua na kuchoshwa na mwenendo ndani ya Chadema.
Akitangaza kujiengua, alisema; "Napenda kuwaambia Wanachadema na Watanzania kwa ujumla, maamuzi haya ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Mkumbo ni maamuzi ya kijuha na yanayowafanya Watanzania sasa waangalie mara mbili mbili kama hawa watu wapo makini na huo ukombozi wanaousema."
Alisema Zitto na wenzake wameonewa, kwani hakuna baya lolote walilolifanya, bali wametoswa kutokana na homa ya uchaguzi mkuu wa ndani ya chama.

"Ni fedheha leo mimi kuwa sehemu ya watu wanaomuita Zitto Kabwe ni msaliti. Siwezi kuendelea na ujinga huu na sipo tayari tena. Si dhambi kumhukumu mtu kwa kuwa anapanga mipango ya kukushinda kwenye uchaguzi, dawa ya mpinzani wako ni kumkabili" Alisema.

Hakuna usaliti, uhaini, Aidha, Chitanda ameeleza kuwa, akiwa mtendaji wa ofisi ya Katibu Mkuu, alishiriki pamoja na Zitto na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa kupanga mikakati mbalimbali, mizuri na mibaya kwa nchi, lakini hawakuwahi kuitwa wasaliti, wahaini wala jina lolote baya.

"Tumekuwa tukiweka mikakati mbalimbali ya ushindi ili chama kishinde, kwa mfano, kabla hata ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki (Jeremiah Sumari), wakati tu ilipobainika anaugua, chama kiliandaa mkakati wa kushinda ubunge wa jimbo hilo na uchaguzi uliporudiwa mkakati ule ulitumika na kushinda.

"Naomba nikiri kwamba nikiwa Katibu wa Sekretarieti tumekuwa tukilazimishwa mara kadhaa kuwashawishi wajumbe wengi kutowaunga mkono watu wenye misimamo thabiti ndani ya chama na badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali za chama kuwajenga wajumbe 'ndio'," alilalamika Chitanda na kudai kuwa, wakati Dk Slaa akisema mjadala wa Zitto umefungwa rasmi, ni uongo kwa kuwa amewaagiza wakurugenzi wa chama kuzunguka nchi nzima kusambaza waraka waliouandaa ukimchafua Zitto.

Kutokana na mambo yanayoendelea ndani ya chama, amedai nafsi yake haipo tayari kuendelea kuwa sehemu ya upotoshaji dhidi ya Watanzania wenzake.
"Nafsi yangu inanikataza kabisa kuendelea kufumbia macho maovu yanayoendelezwa na chama changu. Nafsi yangu imechoka kuendelea kushuhudia ubaguzi wa kidini na kikabila unaofanywa wazi wazi na viongozi wa chama changu.

"Nafsi yangu imekataa sasa, haipo tayari tena kuwa kuwadi wa kuwahadaa Watanzania kuyafikia matarajio tunayowapa ambayo kamwe hayafikiki. Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa Zitto Kabwe na Dk Mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.

"Hivyo basi, nikiwa na akili timamu kabisa, leo tarehe 30.11.2013 nimeamua kujivua nyadhifa zangu zote nilizokuwa nazo ndani ya chama. Sioni tena sababu ya kuendelea kuwa mwanaChadema, sioni tena sababu ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Lindi, sioni tena sababu ya kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu," alisema.
`Kubebana' katika madaraka.

Licha ya kile alichodai ni uonevu dhidi ya Zitto na wenzake, Chitanda pia alilalamikia upendeleo wa nafasi nyeti ndani ya chama kwamba zimekuwa zikiegemea watu wa upande mmoja.
Mathalani, alisema pamoja na uamuzi wa kuwavua madaraka Zitto na wenzake hivi karibuni, Kamati Kuu pia iliridhia uteuzi wa wakurugenzi watano na kuwaongezea pia maslahi.

Aliwataja wakurugenzi hao ni Benson Kigaila (Mkurugenzi wa Oganaizesheni), John Mnyika (Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya Ndani), Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji), John Mrema (Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri) na Wilfred Lwakatare (Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama).

Kwa mujibu wa Chitanda, uteuzi huo hauoneshi sura ya kitaifa kwani kati ya kurugenzi zote sita, nne zinaongozwa na watu wanne kutoka Mkoa mmoja wa Kilimanjaro.
Alisema mabadiliko hayo yanakwenda sambamba na posho nono, akisema wakurugenzi waliokuwa wakilipwa Sh 800,000 kwa mwezi, sasa watakuwa wakilipwa kati ya Sh milioni 1.5 na milioni 2.5 wakati maofisa waandamizi waliokuwa wanalipwa Sh 680,000 sasa watalipwa hadi Sh milioni 1.5.

"Pamoja na kwamba uboreshaji uliridhiwa, lakini katika mpango ulioridhiwa na Baraza Kuu ni pamoja na kulipa posho kwa makatibu wa wilaya na mikoa. Hawa ndio watendaji muhimu katika ujenzi na uhai wa taasisi hii lakini, hawakuangaliwa wala kuguswa badala yake wanatakiwa kujitolea tu kwa hali na mali," alisema.
Tangu uamuzi wa Kamati Kuu wa kuwavua madaraka Zitto na wenzake kwa tuhuma za kupanga mikakati ya `uhaini' ndani ya chama, kumekuwa na mpasuko ndani ya chama, wengine wakiunga mkono uamuzi wa uongozi na wengine wakipinga kwa madai kuwa nguvu kubwa imetumika `kuwaonea' wanasiasa hao vijana, lakini pia wenye nguvu na ushawishi wa kisiasa.

Miongoni mwa wanaotajwa kutoridhika kuondolewa kwa Zitto na wenzake ni mwanazuoni na mkongwe katika duru za kisiasa ambaye pia ni mshauri wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu aliyekaririwa kukionya chama kwa hatua hiyo, akisema haikuwa na ulazima kwa sasa, bali mambo yangeweza kusawazishwa kwa mazungumzo.
Naye Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Temeke na mjumbe wa Baraza Kuu, Patrick Joseph, alitoa kauli iliyodhihirisha kuwa yeye ni mmoja wa wanaomwunga mkono Zitto.
Wengine ni Mwanasheria wa Mbowe, Albert Msando ambaye sasa ni Mwanasheria wa akina Zitto. Wakati Chitanda akiyasema hayo, Ofisa Mwandamizi wa Habari Chadema, Tumaini Makene jana jioni alitoa taarifa inayofafanua madai kadhaa ya Mwenyekiti huyo wa Mkoa wa Lindi aliyejiuzulu.

Katika ufafanuzi wake, alisema hakuna upendeleo katika ugawaji wa madaraka, akisema kati ya wakurugenzi sita waliopo kwa sasa, ni wawili tu ndio wanaotoka Kilimanjaro, Mrema na Komu.
Wengine na mikoa yao ni Mnyika (Mwanza), Kigaila (Dodoma) na Lwakatare (Kagera). Aidha, Makene aliyesema mjadala wa Zitto na wenzake umefungwa na kwamba zinasubiriwa taratibu za kikatiba ndani ya chama, alisema wakurugenzi waliotajwa si wapya katika nafasi zao, bali mpya ni mmoja, ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu. Kibatala ana asili ya Mkoa wa Morogoro.

Amekanusha pia kuwa Chitanda alikuwa Katibu wa Sekretarieti ya Makao Makuu, akisema nafasi hiyo ambayo imo ndani ya Katiba ya Chadema haina mtu mpaka sasa.
"Mahali pengine amejitambulisha kuwa ni Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu. Ofisi hiyo ina Katibu Mtendaji mmoja ambaye ni Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa Chadema," anasema na kuongeza kuwa, kauli ya Chitanda kwamba Zitto na wenzake wameonewa kwa hofu ya uchaguzi inashangaza kwani ni kauli za mara kwa mara zinazotoka kwa mahasimu wa Chadema kisiasa.
Get our toolbar!Get our toolbar!
  • Alexaporn - XXX (+18) Search!Alexaporn - XXX (+18) Search!
 
Sell Your Products At TripleClicks!Share Links Earn Money!
cafepress.com/nicemike
Sale Online!
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger