Marais wa Eac watia saini huko KAMAPALA kuhusu itifaki ya kutumia sarafu moja..!! | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
Labels :
Home » » Marais wa Eac watia saini huko KAMAPALA kuhusu itifaki ya kutumia sarafu moja..!!

Marais wa Eac watia saini huko KAMAPALA kuhusu itifaki ya kutumia sarafu moja..!!

Written By Mike Ntobi on Monday, January 27, 2014 | 10:55 AM

http://www.wavuti.com/uploads/3/0/7/6/3076464/5763105_orig.jpg

L-R ni Marais: Pierre Nkurunzinza (Burundi), Jakaya Mrisho Kikwete (Tanzania), Uhuru Kenyatta (Kenya), Yoweri Museveni (Uganda) na Paul Kagame (Rwanda) muda mfupi baada ya kutia saini itifaki ya Umoja wa Fedha wa Afrika Mashariki (picha: Freddy Maro/IKULU)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo kwa pamoja wametia  saini itifaki ya Umoja wa Fedha  wa Afrika Mashariki, (The East African Monetary Union) katika hoteli ya Speke, Munyonyo  mjini Kampala.

Marais waliotia saini itifaki kwa niaba ya wananchi wao ni Jakaya  Mrisho Kikwete wa Tanzania, Pierre Nkurunziza wa Burundi, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda .

Mara baada ya utiwaji wa saini, itifaki ya Umoja wa Fedha itapelekwa Kwenye mabunge ya nchi wanachama kwa ajili ya 

kuridhia ifikapo Mwezi Julai mwaka 2014.

Utiaji wa saini huu unaanzisha mchakato wa kuelekea kuwa na sarafu moja ifikapo mwaka 2024 kwa nchi za Afrika Mashariki.

Kikao cha viongozi pia kilishuhudia Rais Kenyatta akichukua Uenyekiti wa Jumuiya kutoka kwa Rais Museveni na kuelezea matarajio yake ya Jumuiya  kukua zaidi na kuzitaka nchi wanachama kuelimisha zaidi wananchi wa Afrika Mashariki kuhusu faida za Ushirikiano huu.

Itifaki ya Umoja wa Fedha ni ya tatu baada ya itifaki ya Umoja wa Ushuru wa Forodha na itifaki ya soko la pamoja na hatimaye kuelekea kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki.

Katika mkutano wa Leo, mbele ya viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mwanafunzi Peter Robert kutoka shule ya sekondari Tushikamane, Morogoro amepokea cheti na zawadi ya fedha taslimu baada ya kuibuka mshindi wa shindano la kuandika Insha inayohusu EAC.

Mara baada ya kikao,,Rais Kikwete amerejea jijini Mwanza kuendeleza na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Simiyu ambapo kesho tarehe 1, ataendelea na ziara katika Wilaya ya Busega.

Mwisho.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Kampala, Uganda
30 Nov 2013
Share this article :

Related Posts :

Post a Comment

 
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger