Written By Mike Ntobi on Monday, January 27, 2014 | 10:43 AM
DAKTARI mwenye dhamana ya kituo cha Mkono kwa Mkono ambacho kinachunguza wanawake waliodhalilishwa ikiwemo kubakwa, Dk Marijani Msafiri amesema asilimia 80 ya watoto wa kike wanaoletwa kituoni hapo na wazazi wao , wanafikishwa kuchunguzwa masuala ya ubikira.
Dk Msafiri alisema hayo akizungumza na waandishi wa habari waliotaka kupata maelezo zaidi kuhusu matumizi ya kituo hicho ambacho kimewekwa kwa ajili ya kutoa huduma za haraka kwa wanawake wanaopata matatizo ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa au kulawitiwa.
Alisema kituo hicho kinatumika vibaya kinyume na malengo yake ambapo wazazi wanawalazimisha watoto wa kike kuchunguzwa bikira yao baada ya kuwatilia shaka kwamba wanayo mahusiano ya kimapenzi na wanaume.
"Kituo hiki Mkono kwa Mkono malengo yake ni kutoa huduma za dharura kwa wanawake wanaokabiliwa na matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa.....sasa wazazi wanawaleta watoto wao hapa baada ya kuwatilia shaka kwamba wanamahusiano ya kimapenzi na wanaume kwa ajili ya kuchunguzwa kujua ubikira wao," alisema.
Alisema huo ni aina mpya ya udhalilishaji wa kijinsia kwa sababu wanawake wengi wanapinga kuchunguzwa ubikra huo ambapo kazi hiyo inafanyika kwa nguvu kwa maelekezo ya wazazi tu.
Aidha alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa madaktari wa kufanya vipimo na kuchunguza matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa au kuchunguza ubikra ambapo kazi hizo hufanywa na madaktari wanaume.
Kituo cha Mkono kwa Mkono kilifunguliwa miaka miwili iliyopita ambapo lengo lake kubwa ni kurahisisha kupatikana kwa huduma zote katika kituo kimoja za matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo matukio ya ubakaji.
Kituo hicho kinachotoa huduma zake katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini hapa kinatoa huduma zake kwa ushirikiano mkubwa wa mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia afya na maendeleo ya mtoto na mwanamke ikiwemo UNFPA na UNICEF.
Where does the history of black haircare in this country begin?
“I am a woman who came from the cotton fields of the South. From there I was promoted to the washtub. From there I was promoted to the cook kitchen. And from there I promoted myself into the business of manufacturing hair goods and preparations….I have built my own factory on my own ground.”
~ Madam C.J. Walker
Sarah Breedlove, better known as Madam C.J. Walker, created a successful hair empire in the late 1800′s, including, among other things, scalp conditioners, the permanent wave machine, and the pressing comb. Since those times, black hair and the hair care industry has catapulted to a billion-dollar business.
Here are some of the looks that keep that business booming throughout the decades.
Written By Mike Ntobi on Tuesday, December 17, 2013 | 8:22 AM
Marehemu Nelson Mandela enzi za uhai wake.
MZEE MANDELA ALIACHA WOSIA: WOSIA aliowahi kuuandika hayati Nelson Rolihlahla Mandela 'Mzee Madiba' au 'Tata' (95) enzi za uhai wake akielezea anavyotaka azikwe, ndiyo tishio kubwa lenye utata kuelekea siku ya mazishi yake, Jumapili ijayo, Ijumaa Wikienda limebaini. Mtandao mmoja nchini humo umeukumbushia wosia huo huku familia ikianza kuonesha misimamo tofauti tofauti, hali inayoashiria kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana ndani ya ukoo.
Gari lililobeba mwili wa Nelson Mandela.
FAMILIA INAVYOTAKA: Habari za ndani zilisema kuwa familia inataka mazishi ya kiongozi huyo maarufu duniani yawe makubwa na ya kisasa kwa vile viongozi wa nchi mbalimbali duniani watahudhuria. "Mandela ni kingozi mkubwa sana duniani, mazishi yake lazima yawe makubwa pia ya kisasa. Hawezi kuzikwa kama mwananchi wa kawaida," ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Mmoja wa waombolezaji akigusa picha na Mandela.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa wakati familia hasa wajukuu na watoto wake wakishikilia msimamo huo, wapo wanandugu wanaotaka azikwe kama alivyoandika katika wosia wake huo. SERIKALI YAPANGA MAMBO BILA KUFUATA WOSIA: Habari zaidi zilisema kuwa Serikali ya Afrika Kusini inajitahidi kuupangua wosia huo kwa kuendelea na maandalizi ya mazishi kama haukuwahi kuwepo licha ya kwamba jamii ya watu nchini humo inaheshimu wosia wa marehemu. WOSIA UNAVYOSEMA: Mzee Madiba alishauandika wosia huo kwenye karatasi moja tu ambapo aliagiza anavyotaka azikwe. Alisema kuwa akifa azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake katika Kijiji cha Qunu, Eastern Cape huko 'Sauzi'.
Waombolezaji wakiweka maua katika sanamu la Mandela.
ALITAKA MAZISHI YA KAWAIDA SANA: Inadaiwa wosia huo aliuandika Januari, 1996 wakati bado akiwa rais ambao ulijaa maelekezo yote juu ya mazishi yake. Aliagiza kufanyiwa mazishi ya kawaida sana yenye hadhi ya raia wa kawaida nchini humo hivyo kuyafanya kuwa makubwa na ya kifahari ni kukiuka wosia wa mzee. KABURI ALILOLITAKA MANDELA: Katika wosia wake huo uliotolewa na rafiki yake wa karibu, Mzee Madiba aliandika kuwa akifa azikwe katika eneo la familia lenye makaburi ya ukoo wa Mandela kijijini hapo. Pia aliagiza kuwa kaburi lake liwekewe jiwe la kawaida kama alama ya mahali lilipo ili lisije kupotea kwa mvua au mabadiliko ya tabia nchi.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
ALITAKA KABURI LISISAKAFIWE: Katika tafsiri ya maneno hayo, Mzee Madiba alitaka kaburi lake liwe la kawaida sana, akimaanisha lisijengewe kama ilivyokuwa kwa makaburi ya viongozi wengine wa mfano wake barani Afrika kama, Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Kamuzu Banda (aliyekuwa Rais wa Malawi). WOSIA WAKE ULIKUWA WA UPANDE MMOJA WA KARATASI: Magazeti ya nchini humo, South African Mail na Guardian miezi ya karibuni yaliripoti kumnukuu rafiki huyo wa siku nyingi wa familia ya Mandela akisema: "Madiba hakuwahi kukifanya kifo kuwa jambo kubwa la kufikiriwa, pia hakuwahi kutaka chochote cha fahari wakati wa kumzika." Cha ajabu, wosia huo wa Mandela ulitosha kwenye upande mmoja wa karatasi ya kawaida ya kuandikia licha ya kwamba mauzo ya kitabu chake cha Long Walk to Freedom na michoro yenye jina lake vilimpatia mamilioni ya fedha.
Nelson Mandela (kulia) akiwa na Mwalimu Julius Nyerere enzi za uhai wao.
FAMILIA YACHUKIZWA NA WOSIA: Wosia huo ulielezwa kuwashangaza watu wengi duniani kwani waliamini angekuwa na vitu vingi vya kuandika kulingana na uwezo wake. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, SABC, suala hilo la sehemu atakayozikwa Mzee Madiba liliiudhi mno familia yake akiwemo yule mjukuu wake ambaye ni chifu, Mandla Mandela aliyewahi kufikishwa kortini kwa kuhamisha makaburi hayo ya ukoo na kuyapeleka sehemu nyingine. Pia ndiye msemaji wa familia ya Mandela. DUNIA YAMPINGA MANDELA NA WOSIA WAKE: Baadhi ya wanaharakati ulimwenguni kote walisema wosia huo unapingana na matakwa ya dunia nzima, ambapo walitaka maziko ya mzee huyo yawe makubwa na ya kihistoria ambayo hayajawahi kutokea. Ilifahamika kwamba dunia inataka mazishi hayo yavunje ile rekodi iliyoshikiliwa na mazishi ya Papa John Paul II aliyefariki dunia Aprili 2, 2005.
Mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla Mandela.
SAFARI HII HAKUKIMBIZWA HOSPITALI: Mzee Madiba ambaye alitimiza umri wa miaka 95 Julai 18, mwaka huu, alikuwa hospitalini kwa karibu miezi mitatu nyuma akitibiwa maambukizi kwenye mapafu huku akipumulia mashine. Baadaye alipata nafuu na kurudishwa nyumbani ambako usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita aliugua ghafla na kufariki dunia.
BUY THIS EBOOK NOW! Instant Download Price: $9.99. The whole purpose of revolutionary violence is to destroy at its very roots the institutionalized system of greed which is also the institutionalized system of violence. Today, with the phoney cry of “law and order” the rulers of the imperialist nations attempt to throw the onus of violence on those who are protesting the system under which they live. But the onus is noton them, for violence is the near-monopoly of the state apparatus.
MIKENTOBI Exclusive - For years, inquiring minds have been asking, why R Kelly married an underage Aaliyah, only for the marriage...
Rec
Commt
Deal
INSTANTLY INCREASE YOUR SALES by plugging your products and services into "TRIPLECLICKS!!!" Do you have a merchandise to sell your products? It's Free to list. Pay a fee ONLY when you sell. Sell your product worldwide. Put the marketing muscle of over 100,000 SFI affiliates to work for you, promoting and selling your products in over 190 countries. FREE to Register. Reach millions of potential customers worldwide on the Web. Plug into a new world of customers NOW! at: SIGN UP TODAY FREE!