Kila mtu ambae amefanikiwa kwa kupanda mwenyewe kutoka chini kwenda juu lazima anasimulizi la maisha yake ambalo lina mabonde na milima ya kushangaza kidogo, lakini inavuta usikivu na hisia sana pale msichana mrembo aliyefanikiwa kuwa kati ya list ya juu duniani kimuziki akiwa na simulizi la maisha yake linalotisha ama kuogofya tena akitishwa na yule aliyemzaa.
Jina lake la kuzaliwa ni Onika Tanya Maraj a.k.a Nicki Minaj, first lady wa Young Money mwenye umri wa miaka 30.
Nicki Minaj ali-experience maisha ya kusikitisha hasa katika familia yake mwenyewe iliyomlea, lakini pia mikiki mikiki toka kwa dingi mkorofi ilikuwa balaaa.
Baba yake mzazi alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya kupitiliza, kiasi cha kuwa Teja ajabu, lakini pia alikuwa mkorofi na mkatili sana kitu kilichopelekea wanafamilia hao kuishi kwa uoga na mashaka.
Ilifikia hatua baba Nicki Minaj aliwasha moto kwenye nyumba ya familia hiyo akijaribu kumuua mama yake Nicki Minaj, jaribio ambalo halikufanikiwa.
Lakini Nicki Minaj mwenyewe anasema alijaribu sana kumsaidia mama yake kadri anavyoweza na alitaka awe shupavu sana lakini mama yake hakuweza, Nicki alijiwekea malengo ya kuwa mwenye mafanikio baada ya kufanya kazi ili amsaidie mama yake.
“Siku zote nilikuwa na hiki kitu cha kuwawezeshesha wanawake kwenye akili yangu”, aliliambia jarida la Details, “kwa sababu nilitaka mama yangu awe shupavu, na hakuweza. Niliwaza, kama ntakuwa mwenye mafanikio, Naweza kubadili maisha yake.” Huyo ni Nicki Minaj.
Nicki Minaj alianza kuandika mashairi akiwa na umri wa miaka 12 tu, na baada ya kumaliza La Guardia High School, ambayo inatoa elimu ya sanaa na Muziki aliwaza moja kwa moja kuingia kwenye biashara ya muziki. Alianzia chini na alianza kwa kufanya back up kwa rapperz wa jiji la New York.
Muda mfupi baadae alianza kuandika mashairi yake mwenyewe, na baadae akakutana na Lil Wayne aliyegundua kipaji chake ni silaha ya biashara ya muziki na kumsaini Young Money, ambapo alimsaidia kuifanya mixtape ya “Playtime is Over”, baada ya hapo akaishika dunia na michano yake na kuchukua tuzo kibao zenye heshima duniani, na kupata heshima pia hivi karibuni kuwa jaji wa shindano la kuimba la American Idol wakati album yake ya Pink Friday Roman Reloaded; Re-Up iko sokoni.