“SCENES ZA MAPENZI KWENYE FILAMU ZINAWAUMBUA WASANII WANAONUKA MIDOMO” – IRENE UWOYA | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
Labels :
Home » , » “SCENES ZA MAPENZI KWENYE FILAMU ZINAWAUMBUA WASANII WANAONUKA MIDOMO” – IRENE UWOYA

“SCENES ZA MAPENZI KWENYE FILAMU ZINAWAUMBUA WASANII WANAONUKA MIDOMO” – IRENE UWOYA

Written By Mike Ntobi on Sunday, December 30, 2012 | 10:43 AM



MSANII wa filamu anayejichukulia umaarufu bongo Irene Uwoyaamedai kuwa kuna baadhi ya wasanii wenye majina makubwa wanapenda kucheza filamu za mapenzi na uchezeana huku wakishindwa kuelewa kuwa wananuka midono na mara nyingine huwa wanavumulia pasipo kutoa ukweli huo.

Kauli kama ya msanii huyu iliwahi kutolewa na Janet Jackson kwenye filamu ya ‘Poetic Justice’ iliyozinduliwa mwaka 1993 akimtaka Tupac Shakur kupima vizuri vya ukimwi kwani kuna kipande walitakiwa kuonekana wakipeana midomo kwani walicheza kama wapenzi ndani ya filamu hiyo, ndiyo kitu ambacho hata kwa wasanii wa kitanzania wanatakiwa kujifunza na si kukurupuka kupeana midomo..

Uwoya alisema kuwa kuna sehemu huwa wanakosea na kupeana midomo bila kupima afya kwani wapo wasanii wengine si wasafi na wananuka midomo huku wengine wakiwa wanatumia sana dawa za kulevya hivyo kuna hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa endapo wasipo chukua hatua.

Alisema kuwa wengine wanajijua walivyo lakini wanashindwa kujisafisha na kuwa katika hali nzuri badala yake ndani ya filamu wanaanza kupeanda kiss na kuchezeana bila kujua afya ziko vipi.

“Sasaivi naanza kuwa mkali kwa sababu endapo tukiendelea kuwa kimya tunaweza kujikuta magonjwa yanatukuta hivi hivi” aliongeza.

Hata hivyo msanii huyo aliwashauri baadhi ya wasanii wenye tabia za kupenda kupeana midomo ndani ya filamu wawe makini kwani huwezi jua ni ugonjwa gani anaoweza kupata, na kikubwa zaidi ni kupima kabla ya kazi kuanza ili kama kuna mtu mwenye tatizo apewe tiba mapema.
Share this article :

Related Posts :

Post a Comment

 
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger