01/27/14 | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
[ New Posts ] : Habari Mpya Zote - HAPA CHINI!!!
Labels :

Wafuasi wa CHADEMA waandamana wakimshinikiza Godbless Lema ajiuzulu kwa kuwa jimbo limemshinda

Written By Mike Ntobi on Monday, January 27, 2014 | 11:42 AM


Wafuasi wa CHADEMA jijini Arusha walioambatana na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli Bw. Amani Salenga wakionyesha bango hilo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)..

Amani Salenga akiwa na kundi kubwa la vijana walikutana na waandishi wa habari na kudai kuwa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema ndo chanzo cha vurugu ndani ya CHADEMA kwa kuanzisha kikundi cha vijana kinachohatarisha maisha ya wale wanaopinga na mawazo ya Lema katika utendaji wa chama mkoani Arusha.
 
Amani alisisitiza kuwa kwa kuwa CHADEMA  imeamua kufanya maamuzi kwa maslahi ya watu binafsi hususani swala la viongozi waliovuuliwa vyeo vyao(zitto),basi kila mwanachadema  anatakiwa atambue kuwa ndani ya chama hicho kuna pande mbili , CHADEMA ASILI na CHADEMA FAMILY.


Vijana hao waliokuwa na mabango mbalimbali wamelaani  hatua  ya  chama  chao  kuwafukuza  viongozi  wao  pasipokufuata  katiba  ya  chama  na kusisitiza kuwa Lema ndo tatizo ndani ya Chadema.

JK amuweka kitanzini Profesa Kapuya


RAIS Jakaya Kikwete ameviagiza vyombo vya dola kuhakikisha vinamkamata mtu yeyote bila kujali cheo, atakayebainika kumbaka au kumuoa mwanafunzi wa shule. 
Ametoa kauli hiyo huku aliyekuwa waziri wa wizara tofauti katika awamu mbalimbali za uongozi, Profesa Juma Kapuya, akiandamwa na tuhuma za kumbaka na kutishia kumuua binti, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.
Ingawa Rais Kikwete hakutaja jina, lakini ni dhahiri kuwa kauli hiyo inamgusa pia Profesa Kapuya, Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM).
Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara kwenye wilaya za Itilima, Meatu na Maswa mkoani Simiyu, Rais Kikwete alisema mtu anayefanya mapenzi na wanafunzi lazima akamatwe, ahojiwe na kufunguliwa mashitaka ya ubakaji na si vinginevyo.
"Kuna watu wanafanya mapenzi hadi na wanafunzi wakati sote tunajua ukimwi upo na hauna dawa na unaua. Kwa hiyo kila mmoja wetu awe makini kujikinga nao na tuepuke kuwaambukiza wengine," alisisitiza Rais Kikwete.
Wakati Rais Kikwete akisisitiza wahalifu wa makosa ya kubaka na kuoa wanafunzi wachukuliwe hatua, polisi jijini Dar es Salaam wamekuwa wakisuasua kumchukulia hatua Profesa Kapuya licha ya binti anayedaiwa kumbaka, kufungua jalada namba OB/RB/21124/13 katika kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, akidai kutishiwa kuuawa na mbunge huyo.
Kauli ya Rais Kikwete imeonyesha dhahiri kukerwa na moja ya ujumbe mfupi wa maneno wa simu ya mkononi kutoka kwenye simu inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya kwenda kwa binti aliyebakwa, ambapo mbunge huyo alijigamba kwamba serikali haiwezi kumfanya chochote.
Ujumbe huo unasomeka hivi: "Mkiuawa itakuwa vizuri…itawapunguzia gharama za kuishi, usitake kugombana na serikali mtoto mdogo kama wewe, sisi ndiyo wenye nchi yetu, mwenye hilo gazeti ni Mbowe, sasa mwambieni nyumba ya kuishi si mmemuingizia hela leo?
 Mnatumika tu bure watu wanaingiza hela nyingi, ila mmenitibua lazima niwaue, wiki hii haitaisha, nitapiga kambi kote, jana si wamekuficha, tuone utalindwa milele, maana washatengeneza hela, lazima mvae sanda tu, hilo sio ombi ni wajibu wenu, mnajitia na nyie mafia watoto siyo, watoto wetu wanauza unga nani anawakamata? Nani atapingana  nasi."
Habari kutoka Ikulu ya Rais Kikwete zinaeleza kuwa kiongozi huyo wa nchi amekerwa na kauli ya mbunge huyo wa Urambo Magharibi kwamba serikali haiwezi kumfanya jambo lolote.
Ni kutokana na kauli hiyo, mtoa taarifa wetu alisema rais aliagiza vyombo vya dola kufuatilia kwa karibu sakata hilo na kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake.
Pamoja na msimamo wa Rais Kikwete na binti anayedaiwa kubakwa kuripoti polisi, Profesa Kapuya alifanikiwa kusafiri nje ya nchi huku polisi wakimshuhudia bila kumtia mbaroni.
Akiwa nje ya nchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikaririwa mara kadhaa akijigamba kuwa polisi inamsaka mbunge huyo na itamtia mbaroni mahala popote alipo.
Hata hivyo, Profesa Kapuya alirejea nchini juzi huku polisi wakimshuhudia bila kuchufkua hatua zozote.
Mwanafunzi huyo anadai kubakwa na Profesa Kapuya kwenye moja ya hoteli ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho ndani ya ofisi yake katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipomuita kwenda kuchukua ada.

Hizi Ndio sababu za Wabunifu wa kiume Duniani ni 'Mashoga'...!!

Marc Jacobs

Marc Jacobs
Bila shaka umeshajiuliza sana kwanini wabunifu wengi wa nguo wa kiume duniani ni mashoga. Haya ndio majibu:
Kwanza, tasnia ya mitindo (fashion industry) kiutamaduni imekuwa ikiwakubali zaidi mashoga wanaojulikana wazi (openly gay men) tofauti na fani zingine. Hata leo, ni changamoto kubwa kwa shoga kufikia level ya kuwa CEO ama Mkurugenzi kuliko wanaume wa kawaida.
Tofauti ni kwamba shoga kwenye fashion anaweza kuheshimika na kuenziwa kwenye fani hiyo na kufanikiwa binafsi na kifedha bila kudhihakiwa kama ambavyo anaweza kujikuta akifanyiwa kwenye fani zingine kama upolisi, jeshi na kwenye michezo.

Mifano mizuri inaweza kuwa kwa manguli wa fashion duniani kama Valentino Garavani, Yves Saint Laurent, Perry Ellis, Karl Lagerfeld, Alexander McQueen, Gianni Versace, Alexander Wang, Giorgio Armani, Marc Jacobs (Louis Vuitton) Domenico Dolce na Stefano Gabbana, Tom Ford na wengine. Na hata kwa Tanzania wapo wengi wanaofahamika wazi.

karl-lagerfeld-photographe

Karl Lagerfeld
Japokuwa mambo yanabadilika na hasa kwa nchi za wenzetu na kukubalika kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, kumefanya mashoga nao wafanikiwe kwenye fani zinazotawaliwa na wanaume wa kawaida, lakini mifano ya dunia halisi inabaki michache na hasa tu kwenye majiji ama nchi ambazo mashoga na wasagaji wanapewa heshima sawa na wengine.

Dolce-Gabbana-13

Christian Dior na Cristobal Balenciaga
Pia kihistoria mashoga kwenye fashion walikuwa wakipewa kipaumbele zaidi kuliko wanawake. Ni Coco Chanel pekee ndio alikuwa miongoni mwa wanawake wachache waliofanikiwa kwenye kiwanda hicho kilichokuwa kikitawaliwa zaidi na mashoga Christian Dior na Cristobal Balenciaga.

dolce-and-gabbana

Dolce & Gabbana
Pili, inasemekana kuwa utamaduni wa ushoga huwapa nafasi watu hao uwezo wa ubunifu. Mashujaa kwenye jumuiya ya mashoga sio wachezaji wa soka ama wanajeshi- japo wapo. Lakini zaidi wapo kwenye muziki, uigizaji, utengezaji wa filamu, uandishi na sanaa zingine.
Hii ni kwasababu ya ukweli kwamba hizi ndio zilikuwa kazi ambazo mashoga waliweza kufanikiwa na kuendelea kuwa walivyo na kujivunia wanachokifanya. Uwezo wao wa ubinifu huongezeka na ile sense ya upekee ambayo mashoga huikuza ndani ya ulimwengu wa mapenzi ya jinsia mbili (heterosexual world).

1_(1)-7

Tom Ford
Pointi ya msingi: Upenzi wa mashoga katika urembo, utanashati hauwezi kuelezeka. Inasemekana kuwa mwanaume anayebuni nguo nzuri kwa mwanamke aidha hutaka kuwa na mwanamke ama hutaka kuwa mwanamke'.

Laana!! Binti wa miaka 16 anaswa Akijiuza nyakati za Usiku Akiwa na mtoto mgongoni..!!

Binti (kulia) aliyenaswa akijiuza akiwa na mwanae jijini  Mwanza.

Ama kweli shida haina aibu wala huruma! Binti wa miaka 16 aliyetajwa kwa jina la Mama K, amenaswa laivu akifanya shughuli haramu za uchangudoa akiwa na mwanaye mgongoni, akidai chanzo cha kufanya hivyo ni kutokana na shida inayoiandama familia yake.

Binti huyo alibambwa hivi karibuni akijiuza huku mgongoni akiwa na mwanaye wa mwaka mmoja katika Barabara ya Uhuru (kwenye taa za kuongozea magari), jijini hapa.
Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ambayo imetinga rasmi mkoani hapa ilinasa tukio hilo usiku wa manane ambapo ilifanikiwa kufanya mahojiano na Mama K aliyekuwa na wenzake wengi 
walio chini ya miaka 18.

Paparazi wa OFM akiwa kazini jijini Mwanza.


OFM ilichukua maelezo pamoja na picha za mnato huku wenzake wakitoka nduki baada ya kuona mwanga wa kamera.
Cha kushangaza, wakati akihojiwa na OFM, Mama K alidai kuwa haogopi  kupigwa picha kwa sababu alishanaswa na kuhojiwa runingani kuhusiana na ishu ya kujiuza hivyo siyo ishu kwake na wala haoni aibu.
Huku akiwa na mwanaye mgongoni, binti huyo alidai kuwa amekuwa akijiuza kutokana na ugumu wa maisha. 

OFM: Wewe unatokea maeneo gani na ulianza lini kujiuza? 
Mama K: Mimi ni mwenyeji wa Misungwi (wilaya), kwa hapa mjini naishi Mabatini. Sikumbuki nilianza lini lakini yote hii ni kutokana na ugumu wa maisha. 
OFM: Huyo mtoto mgongoni ni wa kwako? 
Mama K: Ndiyo ni mwanangu wa kumzaa, ana zaidi ya mwaka. Nilijifungua nikiwa na umri wa miaka 15. 
OFM: Baba wa mtoto yuko wapi? 
Mama K: Sijui. 
OFM: Ukipata mteja unamuweka wapi mtoto au unaenda kulala naye na mwanaume?
Mama K: (huku akiondoka) Nawaachia wenzangu.

Katika kujikusanyia data za kutosha, uchunguzi wa OFM uliogusa viunga mbalimbali jijini hapa ulibaini kuwa biashara hiyo haramu imeshika kasi ya ajabu ikihusisha vitoto vidogo kati ya umri wa miaka 12 hadi 16.
Kuhusu bei, tofauti na Dar ambako bei huwa ni ghali, jijini hapa vibinti hivyo vidogo hujiuza kwa kati ya shilingi elfu saba hadi kumi na tano kwa usiku mzima. Hakuna mambo ya 'short time'.
Katika kubainisha ukweli wa mambo kuhusiana na vitendo vya ukahaba ndani ya Jiji la Mwanza, OFM ilimtafuta meya wa jiji hilo ambapo simu yake ya mkononi haikupatikana hewani.

Akizungumzia na gazeti hili kuhusiana na ishu hiyo ya watoto wadogo kujihusisha na biashara hiyo haramu ya ngono, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alikuwa na haya ya kusema:
"Sina taarifa yoyote kuhusiana na watoto hao wanaojiuza ndiyo nasikia kwako labda unipe muda niongee na uongozi wa chini nitalichukulia hatua mara moja.

"Siku Wanawake wakijitambua, Umaarufu wa Diamond MWISHO"....Baby Madaha


MSANII filamu na muziki wa kizazi kipya wa Tanzania Baby Joseph Madaha maarufu kwa jina la (Baby Madaha) amesema kwamba msanii mwenzake wa muziki nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz si msanii bali ni mfanyabiashara.

Madaha amesema kwamba Diamond si mwanamuziki na kamwe huwezi kumlinganisha na msanii kama Barnaba Boy, anayefanya muziki kama sanaa na kazi kulingana na kipaji chake na kwamba Diamond si msanii wa muziki bali ni msanii ngono anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi. 

Baby madaha ambaye hivi sasa yuko nchini Kenya kwa shuguli za muziki amesema kwamba, Diamond hajui kuimba na ndiyo maana amekuwa msanii wa matukio huku nyota yake ikiegemea kwenye mapenzi na wasichana wenye majina makubwa hususn wasanii.

Akizungumza na Mwanahabari katika mahojiano maalum leo baby Madaha alisema kwamba, "Binafsi niliposikia kwamba Diamond anaumiza kichwa kunasa penzi la msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la (Lulu) sikushangaa hata kidogo. kwa sababu nilitambua kwamba soko lake la muziki limeanza kushuka hivyo lazima atafute eneo lingine la kujiimarisha kibiashara, ili jina lake liendelee kuwika".

"Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapo jitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa mwisho wa maisha yake kimuziki,kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaanza kuporomoka"alifafanua Baby Madaha.

Taarifa ya CHADEMA: Ufafanuzi kuhusu tamko la Ndugu A.O. Chitanda



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU A.O. CHITANDA


Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu A.O. Chitanda, huku pia waandishi wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;

Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama, Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, mjadala wake kwa upande wa chama umeshafungwa, huku taratibu za kikatiba za ndani ya chama zikiendelea.

Pili suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni 
wapya;
  1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
  2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).
  3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
  4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
  5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.


Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.

Kama ni suala la kuangalia mtu anatokea wapi (ambalo halijawahi wala haliwezi kuwa moja ya vigezo), ili kuonesha ukweli na kubainisha uongo wa watu wanaojaribu kufanya kazi ya CCM wakisema wao ni wanCHADEMA, kwa kutumia propaganda zile zile na kuzifanya kuwa ni kete zao za kisiasa, tunaweza kutaja maeneo ya wanakotoka au asili yao kama ifuatavyo;

  • Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji, Antony Komu- Kilimanjaro.
  • Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare- Kagera.
  • Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila- Dodoma.
  • Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John John Mnyika- Mwanza
  • Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema- Kilimanjaro.
  • Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala- Morogoro.


Hadi sasa uteuzi wa kurugenzi za Makao Makuu ya CHADEMA haujakamilika. Bado kuna nafasi zinazotakiwa kujazwa kwa kufuata taratibu za chama.

Hii ni kwa sababu restructuring, inayofanyika ndani ya chama, hadi sasa inaendelea katika ngazi ya Makao Makuu na kanda, kisha itaendelea kwa ngazi za mikoa, wilaya, majimbo, kata, kijiji na hatimaye kitongoji.

Katika restructuring hiyo ya nafasi za uteuzi, inayoendelea sasa ambayo inakwenda hatua kwa hatua, hadi kuwa na makatibu wa kuajiriwa ngazi ya chini ya chama, chama kinazingatia uwezo, uadilifu na utayari wa mtu katika kutoa utumishi bora kwa wanaCHADEMA na Watanzania wote katika nafasi husika.

Suala la maslahi ya watumishi wa CHADEMA ni utaratibu wa chama ambao unajadiliwa, kufikiwa uamuzi na kisha kuridhiwa kwenye vikao vya chama, kama ilivyofanyika kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichoketi karibuni.

Katika suala hili la maslahi ya watumishi wanaojitolea Makao Makuu ya CHADEMA ambayo si siri, Ndugu Chitanda amesema uongo mkubwa. Kwanza si kweli kuwa Ofisa Mwandamizi anaweza kulipwa posho kubwa kuliko Mkurugenzi wa kurugenzi husika.

Ndugu huyo anadhihirisha uongo huo yeye mwenyewe kwa kuandika hivi; "800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanzia Tshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs. 6,800,000/= kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni Tshs. 1,000,000-1,500,000/=".

Pia si kweli kuwa kila mtumishi anayejitolea Makao Makuu analipwa. Mathalani, wakurugenzi wenye nafasi za ubunge, hawalipwi hata shilingi moja kwa kazi zote wanazokitumikia chama na Watanzania kwa ujumla.

Kwa maelezo hayo ya kutengeneza, ni kwamba hadi sasa Ofisa Mwandamizi anapokea posho kubwa kuliko Mkurugenzi na hata baada ya 'restructuring' atapata posho kulingana na Mkurugenzi. Anapaswa kuwa mkweli. Mtu anayetaka kuonekana muungwana, anapaswa kujiweka mbali na uongo pamoja, maneno ya kutunga pamoja na upotoshaji wa makusudi.

Kama ilivyoandikwa hapo juu, *restructuring* inaendelea. Ni hatua kwa hatua. Itafika ngazi za chini kama Baraza Kuu lilivyoagiza. Kwa sababu hiyo hadi sasa uteuzi wa Makatibu wa Mikoa na Wilaya haujafanyika.

Hata hivyo ruzuku imekuwa ikipelekwa kila kanda, mkoa, wilaya na jimbo kama ilivyoridhiwa na Kamati Kuu. Na hii ni zaidi ya pikipiki, kompyuta na magari yaliyopelekwa kila kanda. Angelikuwa mkweli, nagelisema na hili pia.

Ndugu Chitanda anajichanganya katika taarifa yake yote. Hii ni moja ya sifa ya kukosa hoja hivyo mtu anaamua kuibua viroja au kutunga maneno kwa sababu ya kushindwa kusema ukweli.

Anaonesha kuwa alikuwa mtu aliyeaminiwa hadi kuwa katika vikao muhimu, lakini wakati huo huo anasema kuna ubaguzi! Tunapaswa kumhurumia kwa kushindwa kuunganisha hata mawazo yake na kupata mtiririko wa hoja zenye mantiki! Angelikuwa mkweli angesema katika vikao vya sekretarieti na CC, aliingiaje kama kuna ubaguzi wa dini!

Kwa sababu anazozijua yeye, Ndugu Chitanda ameamua kujipachika cheo ambacho hajawahi kuwa nacho. Amejiita kuwa ni Katibu wa Sekretarieti ya Makao Makuu.

Ndani ya CHADEMA pamoja na kwamba nafasi hiyo imetajwa ndani ya Katiba ya Chama, hakuna mtu ambaye ameteuliwa kutumikia nafasi hiyo. Kama anaweza athibitishe kwa kutoa barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu Mkuu.

Mahali pengine amejitambulisha kuwa ni Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu. Ofisi hiyo ina Katibu Mtendaji mmoja ambaye ni Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa CHADEMA.

Operesheni ya Chama inayoendelea nchi nzima kwenye majimbo 103, si suala la siri wala lengo bovu kama anavyotaka umma uamini.

Ni mwendelezo wa mpango mkakati wa chama kupitia progamu za Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), unaotekelezwa kwa hatua mbalimbali na kwa mbinu tofauti tofauti pamoja na dhana ya CHADEMA ni msingi.

Operesheni hiyo ambayo ni mwendelezo wa nyingi za namna hiyo zinazokwenda ngazi za chini kabisa za chama, zikilenga kuimarisha taasisi na mifumo, imeanza wiki hii na ilitangazwa mbele ya waandishi wa habari.

Tungependa kumalizia ufafanuzi huu mfupi kwa kutoa tahadhari kwa umma kuwa makini na matamko ya watu wa namna hii. Maana tunajua kwa uhakika yako mengi ya namna hii yatatokea kadri ambavyo Watanzania wanakaribia kuona na kuishi matumaini ya mabadiliko ya kiutawala na mfumo ndani ya nchi yao.

Mathalani katika taarifa yake, Ndugu Chitanda amedhihirisha na kuonesha kuwa ni aina ya watu ambao wanaCHADEMA na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuwaangalia kwa macho ya kuhoji na tahadhari ya hali ya juu, anasema hivi;

"Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda."

Aya hiyo pekee inayotumia lugha wanayotumia mahasimu wa CHADEMA, wakiongozwa na viongozi waaandamizi wa CCM, wanaohangaika kutokana na Watanzania kuwakataa, wakijiandaa kuwaondoa madarakani kwa sababu sera zao zimeshindwa, inatosha kuonesha uhalisia wa taarifa yake yote.

Ni kauli za namna hii (kuwatisha na kutaka kuwatenganisha Watanzania) ambazo zimekuwa zikitumiwa na watawala kama njia pekee ya kutaka kuzuia upepo wa mabadiliko unaovuma nchi nzima, zimekuwa zikiwaunganisha zaidi Watanzania kuiunga mkono CHADEMA bega kwa bega, ili kupata haki na matumaini ya wanyonge, katika mapambano ya awamu ya pili, kuelekea uhuru wa kweli.

Imetolewa leo Novemba 30, 2013, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA

Marais wa Eac watia saini huko KAMAPALA kuhusu itifaki ya kutumia sarafu moja..!!

http://www.wavuti.com/uploads/3/0/7/6/3076464/5763105_orig.jpg

L-R ni Marais: Pierre Nkurunzinza (Burundi), Jakaya Mrisho Kikwete (Tanzania), Uhuru Kenyatta (Kenya), Yoweri Museveni (Uganda) na Paul Kagame (Rwanda) muda mfupi baada ya kutia saini itifaki ya Umoja wa Fedha wa Afrika Mashariki (picha: Freddy Maro/IKULU)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo kwa pamoja wametia  saini itifaki ya Umoja wa Fedha  wa Afrika Mashariki, (The East African Monetary Union) katika hoteli ya Speke, Munyonyo  mjini Kampala.

Marais waliotia saini itifaki kwa niaba ya wananchi wao ni Jakaya  Mrisho Kikwete wa Tanzania, Pierre Nkurunziza wa Burundi, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda .

Mara baada ya utiwaji wa saini, itifaki ya Umoja wa Fedha itapelekwa Kwenye mabunge ya nchi wanachama kwa ajili ya 

kuridhia ifikapo Mwezi Julai mwaka 2014.

Utiaji wa saini huu unaanzisha mchakato wa kuelekea kuwa na sarafu moja ifikapo mwaka 2024 kwa nchi za Afrika Mashariki.

Kikao cha viongozi pia kilishuhudia Rais Kenyatta akichukua Uenyekiti wa Jumuiya kutoka kwa Rais Museveni na kuelezea matarajio yake ya Jumuiya  kukua zaidi na kuzitaka nchi wanachama kuelimisha zaidi wananchi wa Afrika Mashariki kuhusu faida za Ushirikiano huu.

Itifaki ya Umoja wa Fedha ni ya tatu baada ya itifaki ya Umoja wa Ushuru wa Forodha na itifaki ya soko la pamoja na hatimaye kuelekea kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki.

Katika mkutano wa Leo, mbele ya viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mwanafunzi Peter Robert kutoka shule ya sekondari Tushikamane, Morogoro amepokea cheti na zawadi ya fedha taslimu baada ya kuibuka mshindi wa shindano la kuandika Insha inayohusu EAC.

Mara baada ya kikao,,Rais Kikwete amerejea jijini Mwanza kuendeleza na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Simiyu ambapo kesho tarehe 1, ataendelea na ziara katika Wilaya ya Busega.

Mwisho.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Kampala, Uganda
30 Nov 2013

CHADEMA yazidi kupukutika...Mwekiti wa chama Mkoani Lindi nae Ajiengua, Anena Siri Nzito kuhusu Chama hicho..!!



SASA ni dhahiri kwamba hali si shwari ndani ya Chadema, baada ya viongozi zaidi kuendelea kuachia ngazi kwa kile walichodai kuchoshwa na hali ya mambo katika chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Said Arfi kujiuzulu wadhifa wake mwishoni mwa wiki iliyopita, jana ilikuwa zamu ya Mwenyekiti wa Chadema mkoani Lindi, Ally Chitanda aliyetangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya chama na pia kujivua uanachama.
Mbali ya kuwa Mwenyekiti wa Mkoa, kabla ya uamuzi wake huo uliotangazwa jana, Chitanda pia alikuwa Katibu wa Sekretarieti katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema Taifa katika makao yake makuu yaliyopo Mtaa wa Togo, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Alikuwa pia Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.
Chitanda alianika uamuzi wake huo jana katika mkutano wake na wanahabari mjini Lindi, akisema amechoshwa na unafiki na uonevu unaoendelea ndani ya chama hicho alichojiunga nacho miaka kumi iliyopita akitokea NCCR-Mageuzi.

Alisema kikao cha Kamati Kuu kilichoketi kwa siku mbili na kufikia maazimio kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwavua madaraka Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto, Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ndiyo yaliyomchefua na kuchoshwa na mwenendo ndani ya Chadema.
Akitangaza kujiengua, alisema; "Napenda kuwaambia Wanachadema na Watanzania kwa ujumla, maamuzi haya ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Mkumbo ni maamuzi ya kijuha na yanayowafanya Watanzania sasa waangalie mara mbili mbili kama hawa watu wapo makini na huo ukombozi wanaousema."
Alisema Zitto na wenzake wameonewa, kwani hakuna baya lolote walilolifanya, bali wametoswa kutokana na homa ya uchaguzi mkuu wa ndani ya chama.

"Ni fedheha leo mimi kuwa sehemu ya watu wanaomuita Zitto Kabwe ni msaliti. Siwezi kuendelea na ujinga huu na sipo tayari tena. Si dhambi kumhukumu mtu kwa kuwa anapanga mipango ya kukushinda kwenye uchaguzi, dawa ya mpinzani wako ni kumkabili" Alisema.

Hakuna usaliti, uhaini, Aidha, Chitanda ameeleza kuwa, akiwa mtendaji wa ofisi ya Katibu Mkuu, alishiriki pamoja na Zitto na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa kupanga mikakati mbalimbali, mizuri na mibaya kwa nchi, lakini hawakuwahi kuitwa wasaliti, wahaini wala jina lolote baya.

"Tumekuwa tukiweka mikakati mbalimbali ya ushindi ili chama kishinde, kwa mfano, kabla hata ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki (Jeremiah Sumari), wakati tu ilipobainika anaugua, chama kiliandaa mkakati wa kushinda ubunge wa jimbo hilo na uchaguzi uliporudiwa mkakati ule ulitumika na kushinda.

"Naomba nikiri kwamba nikiwa Katibu wa Sekretarieti tumekuwa tukilazimishwa mara kadhaa kuwashawishi wajumbe wengi kutowaunga mkono watu wenye misimamo thabiti ndani ya chama na badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali za chama kuwajenga wajumbe 'ndio'," alilalamika Chitanda na kudai kuwa, wakati Dk Slaa akisema mjadala wa Zitto umefungwa rasmi, ni uongo kwa kuwa amewaagiza wakurugenzi wa chama kuzunguka nchi nzima kusambaza waraka waliouandaa ukimchafua Zitto.

Kutokana na mambo yanayoendelea ndani ya chama, amedai nafsi yake haipo tayari kuendelea kuwa sehemu ya upotoshaji dhidi ya Watanzania wenzake.
"Nafsi yangu inanikataza kabisa kuendelea kufumbia macho maovu yanayoendelezwa na chama changu. Nafsi yangu imechoka kuendelea kushuhudia ubaguzi wa kidini na kikabila unaofanywa wazi wazi na viongozi wa chama changu.

"Nafsi yangu imekataa sasa, haipo tayari tena kuwa kuwadi wa kuwahadaa Watanzania kuyafikia matarajio tunayowapa ambayo kamwe hayafikiki. Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa Zitto Kabwe na Dk Mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.

"Hivyo basi, nikiwa na akili timamu kabisa, leo tarehe 30.11.2013 nimeamua kujivua nyadhifa zangu zote nilizokuwa nazo ndani ya chama. Sioni tena sababu ya kuendelea kuwa mwanaChadema, sioni tena sababu ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Lindi, sioni tena sababu ya kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu," alisema.
`Kubebana' katika madaraka.

Licha ya kile alichodai ni uonevu dhidi ya Zitto na wenzake, Chitanda pia alilalamikia upendeleo wa nafasi nyeti ndani ya chama kwamba zimekuwa zikiegemea watu wa upande mmoja.
Mathalani, alisema pamoja na uamuzi wa kuwavua madaraka Zitto na wenzake hivi karibuni, Kamati Kuu pia iliridhia uteuzi wa wakurugenzi watano na kuwaongezea pia maslahi.

Aliwataja wakurugenzi hao ni Benson Kigaila (Mkurugenzi wa Oganaizesheni), John Mnyika (Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya Ndani), Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji), John Mrema (Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri) na Wilfred Lwakatare (Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama).

Kwa mujibu wa Chitanda, uteuzi huo hauoneshi sura ya kitaifa kwani kati ya kurugenzi zote sita, nne zinaongozwa na watu wanne kutoka Mkoa mmoja wa Kilimanjaro.
Alisema mabadiliko hayo yanakwenda sambamba na posho nono, akisema wakurugenzi waliokuwa wakilipwa Sh 800,000 kwa mwezi, sasa watakuwa wakilipwa kati ya Sh milioni 1.5 na milioni 2.5 wakati maofisa waandamizi waliokuwa wanalipwa Sh 680,000 sasa watalipwa hadi Sh milioni 1.5.

"Pamoja na kwamba uboreshaji uliridhiwa, lakini katika mpango ulioridhiwa na Baraza Kuu ni pamoja na kulipa posho kwa makatibu wa wilaya na mikoa. Hawa ndio watendaji muhimu katika ujenzi na uhai wa taasisi hii lakini, hawakuangaliwa wala kuguswa badala yake wanatakiwa kujitolea tu kwa hali na mali," alisema.
Tangu uamuzi wa Kamati Kuu wa kuwavua madaraka Zitto na wenzake kwa tuhuma za kupanga mikakati ya `uhaini' ndani ya chama, kumekuwa na mpasuko ndani ya chama, wengine wakiunga mkono uamuzi wa uongozi na wengine wakipinga kwa madai kuwa nguvu kubwa imetumika `kuwaonea' wanasiasa hao vijana, lakini pia wenye nguvu na ushawishi wa kisiasa.

Miongoni mwa wanaotajwa kutoridhika kuondolewa kwa Zitto na wenzake ni mwanazuoni na mkongwe katika duru za kisiasa ambaye pia ni mshauri wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu aliyekaririwa kukionya chama kwa hatua hiyo, akisema haikuwa na ulazima kwa sasa, bali mambo yangeweza kusawazishwa kwa mazungumzo.
Naye Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Temeke na mjumbe wa Baraza Kuu, Patrick Joseph, alitoa kauli iliyodhihirisha kuwa yeye ni mmoja wa wanaomwunga mkono Zitto.
Wengine ni Mwanasheria wa Mbowe, Albert Msando ambaye sasa ni Mwanasheria wa akina Zitto. Wakati Chitanda akiyasema hayo, Ofisa Mwandamizi wa Habari Chadema, Tumaini Makene jana jioni alitoa taarifa inayofafanua madai kadhaa ya Mwenyekiti huyo wa Mkoa wa Lindi aliyejiuzulu.

Katika ufafanuzi wake, alisema hakuna upendeleo katika ugawaji wa madaraka, akisema kati ya wakurugenzi sita waliopo kwa sasa, ni wawili tu ndio wanaotoka Kilimanjaro, Mrema na Komu.
Wengine na mikoa yao ni Mnyika (Mwanza), Kigaila (Dodoma) na Lwakatare (Kagera). Aidha, Makene aliyesema mjadala wa Zitto na wenzake umefungwa na kwamba zinasubiriwa taratibu za kikatiba ndani ya chama, alisema wakurugenzi waliotajwa si wapya katika nafasi zao, bali mpya ni mmoja, ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu. Kibatala ana asili ya Mkoa wa Morogoro.

Amekanusha pia kuwa Chitanda alikuwa Katibu wa Sekretarieti ya Makao Makuu, akisema nafasi hiyo ambayo imo ndani ya Katiba ya Chadema haina mtu mpaka sasa.
"Mahali pengine amejitambulisha kuwa ni Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu. Ofisi hiyo ina Katibu Mtendaji mmoja ambaye ni Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa Chadema," anasema na kuongeza kuwa, kauli ya Chitanda kwamba Zitto na wenzake wameonewa kwa hofu ya uchaguzi inashangaza kwani ni kauli za mara kwa mara zinazotoka kwa mahasimu wa Chadema kisiasa.

BIKIRA kwa wasichana yageuka kitu 'adimu' huko Zanzibar..!!

Photo

DAKTARI mwenye dhamana ya kituo cha Mkono kwa Mkono ambacho kinachunguza wanawake waliodhalilishwa ikiwemo kubakwa, Dk Marijani Msafiri amesema asilimia 80 ya watoto wa kike wanaoletwa kituoni hapo na wazazi wao , wanafikishwa kuchunguzwa masuala ya ubikira.

Dk Msafiri alisema hayo akizungumza na waandishi wa habari waliotaka kupata maelezo zaidi kuhusu matumizi ya kituo hicho ambacho kimewekwa kwa ajili ya kutoa huduma za haraka kwa wanawake wanaopata matatizo ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa au kulawitiwa.

Alisema kituo hicho kinatumika vibaya kinyume na malengo yake ambapo wazazi wanawalazimisha watoto wa kike kuchunguzwa bikira yao baada ya kuwatilia shaka kwamba wanayo mahusiano ya kimapenzi na wanaume.

"Kituo hiki Mkono kwa Mkono malengo yake ni kutoa huduma za dharura kwa wanawake wanaokabiliwa na matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa.....sasa wazazi wanawaleta watoto wao hapa baada ya kuwatilia shaka kwamba wanamahusiano ya kimapenzi na wanaume kwa ajili ya kuchunguzwa kujua ubikira wao," alisema.

Alisema huo ni aina mpya ya udhalilishaji wa kijinsia kwa sababu wanawake wengi wanapinga kuchunguzwa ubikra huo ambapo kazi hiyo inafanyika kwa nguvu kwa maelekezo ya wazazi tu.
Aidha alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa madaktari wa kufanya vipimo na kuchunguza matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa au kuchunguza ubikra ambapo kazi hizo hufanywa na madaktari wanaume.

Kituo cha Mkono kwa Mkono kilifunguliwa miaka miwili iliyopita ambapo lengo lake kubwa ni kurahisisha kupatikana kwa huduma zote katika kituo kimoja za matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo matukio ya ubakaji.

Kituo hicho kinachotoa huduma zake katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini hapa kinatoa huduma zake kwa ushirikiano mkubwa wa mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia afya na maendeleo ya mtoto na mwanamke ikiwemo UNFPA na UNICEF.
Get our toolbar!Get our toolbar!
  • Alexaporn - XXX (+18) Search!Alexaporn - XXX (+18) Search!
 
Sell Your Products At TripleClicks!Share Links Earn Money!
cafepress.com/nicemike
Sale Online!
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger