"Siku Wanawake wakijitambua, Umaarufu wa Diamond MWISHO"....Baby Madaha | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
Labels :
Home » » "Siku Wanawake wakijitambua, Umaarufu wa Diamond MWISHO"....Baby Madaha

"Siku Wanawake wakijitambua, Umaarufu wa Diamond MWISHO"....Baby Madaha

Written By Mike Ntobi on Monday, January 27, 2014 | 11:05 AM


MSANII filamu na muziki wa kizazi kipya wa Tanzania Baby Joseph Madaha maarufu kwa jina la (Baby Madaha) amesema kwamba msanii mwenzake wa muziki nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz si msanii bali ni mfanyabiashara.

Madaha amesema kwamba Diamond si mwanamuziki na kamwe huwezi kumlinganisha na msanii kama Barnaba Boy, anayefanya muziki kama sanaa na kazi kulingana na kipaji chake na kwamba Diamond si msanii wa muziki bali ni msanii ngono anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi. 

Baby madaha ambaye hivi sasa yuko nchini Kenya kwa shuguli za muziki amesema kwamba, Diamond hajui kuimba na ndiyo maana amekuwa msanii wa matukio huku nyota yake ikiegemea kwenye mapenzi na wasichana wenye majina makubwa hususn wasanii.

Akizungumza na Mwanahabari katika mahojiano maalum leo baby Madaha alisema kwamba, "Binafsi niliposikia kwamba Diamond anaumiza kichwa kunasa penzi la msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la (Lulu) sikushangaa hata kidogo. kwa sababu nilitambua kwamba soko lake la muziki limeanza kushuka hivyo lazima atafute eneo lingine la kujiimarisha kibiashara, ili jina lake liendelee kuwika".

"Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapo jitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa mwisho wa maisha yake kimuziki,kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaanza kuporomoka"alifafanua Baby Madaha.
Share this article :

Related Posts :

Post a Comment

 
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger