KESI YA LULU MICHAEL YASAJILIWA RASMI MAHAKAMA KUU | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
Labels :
Home » , » KESI YA LULU MICHAEL YASAJILIWA RASMI MAHAKAMA KUU

KESI YA LULU MICHAEL YASAJILIWA RASMI MAHAKAMA KUU

Written By Mike Ntobi on Sunday, December 30, 2012 | 9:04 AM



Kesi ya mauaji ya kutokukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael `Lulu’, imepokelewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kusajiliwa kwa namba 125 ya mwaka 2012.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mahakamani hapo, kesi hiyo imepokelewa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na inasubiri kupangiwa Jaji na tarehe ya kuanza kusikilizwa.

Awali Lulu alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, kwa kukusudia lakini baada ya upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi alibadilishiwa mashitaka na kuwa kuua bila kukusudia.

Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu  Augustina Mmbando, katika hatua za awali na Lulu hakuruhusiwa kujibu mashitaka yanayomkabili kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Kwa mujibu wa sheria, kutokana na Lulu kushitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia, anaweza kupata dhamana.
Share this article :

Related Posts :

Post a Comment

 
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger