May 2013 | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
[ New Posts ] : Habari Mpya Zote - HAPA CHINI!!!
Labels :

BINTI ATOROKEA UINGEREZA AKIKWEPA KUTOMASWA NA MFALME MSWATI

Written By Mike Ntobi on Friday, May 24, 2013 | 2:46 PM



Hapa King Mswati III akiwa na mmoja wa wake zake aliyemchagua katika sherehe za kuchagua na kuoa mke mpya (Kigori au Bikira) zinazofanyika kila mwaka nchini Swaziland.

Msichana mdogo ameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza baada ya kukataa kwa dharau harakati za ndoa za wake wengi za Mfalme Mswati III wa Swaziland na kugoma kujiunga kwenye nyumba harimu ya wake 13.

Tintswalo Ngobeni, mwenye umri wa miaka 22, alitimkia Uingereza kutoka taifa hilo la kusini mwa Afrika akiwa na umri wa chini ya miaka 18 baada ya kuvuta hisia za mfalme huyo milionea, mtawala maarufu mkandamizaji kwa maisha yake ya anasa.


Ikiwa ni sehemu ya mila za Swazi, Mfalme Mswati III, mwenye umri wa miaka 45, anaruhusiwa kuchagua mke mpya kila mwaka.
  
Tintswalo, ambaye sasa anaishi mjini Birmingham, alikuwa na umri wa miaka 15 tu wakati Mfalme huyo alipofanya harakati zake baada kumuona kwenye jumba la kifalme la mke wake wa nne, LaNgangaza. Binti huyo alisema 'alitishika' pale alipogundua dhamira zake za ndoa.

Aliongeza: "Alianza kunipigia simu kwenye shule ya bweni. Aliniuliza kama ningetaka kuwa sehemu ya familia ya kifalme. Ilinibidi kukaa kimya kuhusu mashaka yangu lakini nilifahamu sikutaka kuolewa naye na kujitolea maisha yangu kwa mfalme huyo.

"Wake zake wamewekwa kwenye majumba yao, wakizingirwa na walinzi, na hakika hawawezi kwenda kokote isipokuwa tu mfalme akisema hivyo. Kitu pekee wanachofanya ni kwenda Marekani mara moja kwa mwaka, wakati mfalme huyo anapowapatia posho kwa ajili ya manunuzi."

Tintswalo alikuwa amelazimishwa kuachana na maisha ya starehe kwenye shule moja ya bweni huku shangazi yake, ambaye alikuwa mlezi wake mkuu, akisuka mipango ya kutorokea Uingereza kuungana na mama yake, ambaye alihamia mjini Birmingham miaka mitano kabla, akimtoroka mume wake mnyanyasaji.

"Sikuwa na jinsi," alisema. "Hakuna aliyewahi kumwangusha mfalme huyo au kuthubutu kumdharau, hivyo nikatoweka tu."

Tangu kuwasili nchini Uingereza, Tintswalo amekuwa sauti ya upinzani dhidi ya utawala kandamizi za Swazi, ambapo vyama vya upinzani vya siasa vimefungiwa na wanaharakati wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara au kushambuliwa.

Hatahivyo, shughuli kuu za Tintswalo, ikiwamo maandamano ya kila wiki nje ya ubalozi wa Swazi mjini London akiwa na kikundi cha Swazi Vigil, zimesikika kwa mamlaka hizo nchini kwake na sasa anaamini yuko kwenye hatari kubwa zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.

Alisema: "Hivi karibuni nilipata taarifa kwamba watu wametumwa kutoka Swaziland kuja kunikamata, jambo ambalo hakika linanitisha mno. Kama nikirejea, nitakamatwa au mbaya zaidi huku pale kuna watu ambao wanateseka, kupigwa au kuuawa kwa kujihusisha na siasa."
  
Tintswalo sasa anaishi katika mashaka ya kuweza kurejea nchini Swaziland, baada ya ombi lake la kwanza la hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza mwaka 2007 kukataliwa mwaka 2011.

Mwezi uliopita, alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha kushikilia wahamiaji baada ya miezi 18 ya kuripoti kila wiki katika mamlaka hizo.
 

Hatahivyo, baada ya shinikizo kutoka TUC na ofisi ya Mbunge wa Birmingham kupitia chama cha Labour, Roger Godsiff, Tintswalo aliachiwa na sasa amekata rufaa wizara ya Mambo ya Ndani.
 

Godsiff alisema juzi: "Tumefurahishwa mno wanasheria walifanikiwa sana katika kuwezesha kutazamwa upya kwa kesi ya Ngobeni."

Baba huyo wa wake 13 na watoto 27, Mfalme Mswati III alikuwa mgeni kwenye harusi ya William na Kate na pia kwenye sherehe za Miaka 50 ya Malkia wakati wa majira ya joto mwaka jana.











Mke wa sita wa mfalme huyo alitoroka kutoka kwenye jumba hilo harimu mwaka jana, akielezea miaka kadhaa ya 'machungu na udhalilishaji wa kimwili' uliofanywa na mume wake. 
  
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani alikataa kuzungumzia chochote.

Mikakati ya CHADEMA kuteka waandishi; hapa Lwakatare alikuwa anamaanisha nini?



Mikakati ya CHADEMA kuteka waandishi

Wakuu nimeipata hii youtube, inatisha na huwezi kuamini.

mikakati mikubwa inachorwa na kutekelezwa na watu tunaowaamini ni wanamapinduzi na wanamageuzi.

Hii sasa hatari.

Jionee na kusikiliza mwenyewe ukweli huu kutoka kwenye youtube. Huyu anayeongea na kupanga mikakati ni MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA WA CHADEMA WILLIFRED LWAKATARE akitoa maelekezo kwa vijana wake kwenda kutekeleza tukio la kumteka mwandishi mwandamizi wa mwananchi ambaye ni threat kubwa kwa CHADEMA na ambaye ni rafiki mkubwa wa Zitto.

Anatolea mfano wa matukio mengine waliyoyatekeleza kama lile la kumwagiwa tindikali MUSSA TESHA huko Igunga na kuuawa kwa kijana katika vurugu za CHADEMA na polisi huko Morogoro ambapo tuliambiwa ameangukiwa na kitu chenye ncha kali...

Kwa kipindi cha miaka miwili mitatu sasa kumekuwa na matukio ya kinyama na ya uvunjaji haki za binadamu dhidi ya watanzania wachache wenye moyo wa uzalendo wa kuleta haki na usawa kwa jamii ya kitanzania iliyonyanyasika kwa kipindi kirefu.

Hivi majuzi Absalom kibanda mwenyekiti wa jukwaa la wahariri ameteswa na kufanyiwa unyama wa hali ya juu huku jamii ikibaki na maswali yasiyokuwa na majibu.

Aliteswa mpiganaji DR ULIMBOKA wakati yupo kwenye harakati za kuitetea sekta ya afya hapa nchini.

kijana ISSAH alimwagiwa tindikali huko igunga huku kukitokea mauaji ya kusikitisha ya mwandishi DAUDI MWANGOSI mkoani iringa na mwananchi asiye na hatia huko morogoro.

Watu wenye uchungu na nchi yao wamechoka wameona sasa basi...

Tukio la KIBANDA ni mwendelezo wa matukio yanayofuata.. Hivi karibuni mtasikia tukio lingine kubwa dhidi ya mwandishi mwandamizi wa Mwananchi Communications Ltd...... sikiliza video.

Huyu anayeongea ni mchora dili mkuu kwa maelekezo ya mwenyekiti na katibu wake mkuu. 

Hii ni part 4, part zingine zimekwisha tekelezwa Ila ZITAWEKWA HAPA WAKATI MAHSUSI UKIFIKA...

CHADEMA, hapa Lwakatare alikuwa anamaanisha nini?

BOMB SHELL CHADEMA na UTEKAJI NYARA WAANDISHI

Wakuu naomba tutafakari kwa kina hii video ya mkakati wa utekaji nyara ambao ulikua ukielezewa hapa kwenye video na mkuu wa kitengo cha usalama (utekeji) ndani ya chadema, huyu ni Wilfred Lwakatare zamani alikua akifanya kazi na CUF, Je hapa alikua akim-target nani??????????????????????????????? je ni Dk Ulimboka?? je ni Kibanda??.
 Naona kuna jamaa anasemwa kuwa ni mkali wa kuchonga plan lakini haonekani mahali!!!
This may turn out to be very interesting...
Kutokana na hii clip naanza kupata mwanga.... Huyo aliyeiposti hii clip LAZIMA atakakuwa kwa njia moja ama nyingine anahusika. Baada ya kuipata, akaamua kumshambulia Kibanda ili ionekane mzungumzaji kwenye hii clip ndie muuaji.... Kwa hiyo hata Ridhiwani alipoposti ile kejeli facebook alikuwa na maana kubwa sana na huenda anajua undani wa kila kitu... Undani ni kwamba kitengo cha usalama (utekaji) chadema kinahusika sana,inabidi turudi nyuma mpaka kwenye kifo cha chacha wangwe,pengine huyu bwana ndio ali-engineer ile "ajali".
It's not gonna help either, all in all huyo anaezungumza ni mkuu wa kitengo cha usalama (utekaji) cha chadema, anaitwa Wilfred Lwakatare, that is a reality, sio tetesi.. unless aikane video hii, sura yake na sauti yake! Michango naona imepungua kwa kuwa Chadema kwa video hii imeshikwa pabaya, na naishangaa polisi kumuacha huyu muuaji akiendelea kutamba licha ya ushahidi huu wa wazi
Ila cha muhimu, "Hizi zote ni nadharia". Ili zithibitike inabidi polisi watoe taarifa ya uchunguzi wao kwanza.

Yuko mtu mmoja yeye alijaribu kuwa tofauti na clip hii, na anasema "Magamba hata mfanyeje, hamtaweza kuubadilisha ukweli uliopo akilini mwa watanzania kwamba Dr. Ulimboka na Kibanda wametekwa na Mbwa wa Magamba na nyie mitakataka mnaokuja kuandika upuuzi ili kutaka kuwapoteza watu, subirini ukombozi ukifika, hamtatutoroka!"

============================== ============================
MANENO YALIYOANDIKWA KUAMBATANA NA VIDEO YANASOMEKA HIVI:
============================== ============================

Published on Mar 12, 2013 

Video; mikakati ya mateso ya kibanda na mwandishi mwandamizi wa gazeti la mwananchi; mhusika mkuu huyu hapa. Kwa muda sasa hapa tanzania kumekuwepo na matukio ya kusikitisha ya kuteka na kutesa wanaharakati wa haki za binadamu akina mwangosi, ulimboka na wengine..

Sisi wazalendo na wapenda amani ya tanzania tunasema tumechoka na sasa basi tunaweka wazi kila kitu ili umma ujue kinachoendelea..kweli daima itakuweka huru... video hii inaonyesha sehemu tu ya matukio yaliyokwishatekelezwa na chadema , mpango mzima ukiratibiwa na mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama willifred lwakatare kwa maelekezo ya mwenyekiti mh.

Mbowe na katibu mkuu dr slaa. Katika video hii lwakatare anatoa maelekezo kwa kijana wake kwenda kutekeleza utekaji wa mwandishi wa kampuni ya mwananchi huku akitolea mfano wa matukio ambayo chama kiliyatekeleza kama lile la igunga ambapo mussa tesha alimwagiwa tindikali na lile la morogoro ambapo kijana mmoja alifariki katika vurugu za maandamano ya chadema ambapo polisi walitoa taarifa kuwa kijana huyo ameangukiwa na kitu kizito. Hii video ni sehemu tu ya video zingine ambazo tutazitoa wakati muafaka ukifika..
Get our toolbar!Get our toolbar!
  • Alexaporn - XXX (+18) Search!Alexaporn - XXX (+18) Search!
 
Sell Your Products At TripleClicks!Share Links Earn Money!
cafepress.com/nicemike
Sale Online!
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger