NDEGE ILIYOTUA KWA DHARULA ARUSHA YAFANIKIWA KURUKA [Video] | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
Labels :
Home » , , » NDEGE ILIYOTUA KWA DHARULA ARUSHA YAFANIKIWA KURUKA [Video]

NDEGE ILIYOTUA KWA DHARULA ARUSHA YAFANIKIWA KURUKA [Video]

Written By Mike Ntobi on Saturday, December 21, 2013 | 7:25 PM

Hatimaye ndege ya Shirika la Ethiopian Airlines iliyotua kwa dharura uwanja mdogo wa Arusha juzi ikiwa na abiria 200 imefanikiwa kuruka kuendelea na safari yake salama wa salimini.

Angalia Video hapo chini jinsi ndege ilivyofanikiwa kuruka baada ya kufanyiwa marekebisho madogo baada ya kutua kwa dhalura huko Arusha katika uwanja mdogo wa ndege.




Ndege aina ya Boeing 767 inayosadikiwa kuwa ni ya Shirika la Ndege la Ethiopia imetua kwa dharura majira ya saa tisa alasiri katika kiwanja cha kurushia ndege ndogo cha Arusha badala ya kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, KIA. 



Abiria zaidi ya mia mbili (200) waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamenusurika kifo, wanasubiri msaada ngazi waweze kushushwa. 



Watu wakiangalia jinsi ndege hiyo ilivyonusurika kupata ajali mbaya baada ya kufika mwisho wa Runway.


Watu wakiangalia jinsi ndege hiyo ilivyonusurika kupata ajali mbaya baada ya kufika mwisho wa Runway na Rubani kuamua kuikatisha kuelekea kwenye eneo lenye majani ili kuinusuru ndege pamoja na abiria wake.


Hapa ndege hiyo kubwa aina ya Boeing 767 ikionekana imeacha Runway (lami) na kujikita kwenye eneo lenye majani na udongo tu.


Hapa ndege hiyo kubwa aina ya Boeing 767 ikiwa imejichimbia chini tairi ya mbele baada ya kuwa Rubani ameona ndege imefika mwisho wa uwanja na ndege bado ina kasi, hivyo kwa utaalamu ana ufundi wa hali ya juu, Rubani huyo aliikatisha kona ndege kuelekea eneo lenye majani na udongo kutoka pale ilipoishia lami.
Share this article :

Related Posts :

Post a Comment

 
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger