December 2012 | MIKENTOBI MIKENTOBI - A Blog with updated posts about events and current issues!
NEWS UPDATE :
Over a 100,000 ways to Earn Online!Sale Online!
[ New Posts ] : Habari Mpya Zote - HAPA CHINI!!!
Labels :

HII NDO MAKALA ILIYOSABABISHA "MHARIRI MTENDAJI WA TANZANIA DAIMA" AFIKISHWE MAHAKAMANI

Written By Mike Ntobi on Monday, December 31, 2012 | 11:53 PM


Na Samson Mwigamba


MAKALA hii ilikuwa itoke Jumatano ya wiki iliyopita lakini kwa sababu za kiufundi ikashindikana. Imekuwa ni bahati nzuri kwamba inapotoka leo, ijibu swali la askari polisi dereva wa gari la maji ya kuwasha.

Askari huyo alimweleza Mwalimu Mkuu wa watu jinsi roho inavyomuuma pale anapowamwagia Watanzania wenzake maji hayo ya kuwasha wakati wakidai haki yao. Askari uliyeuliza na wenzako wote someni makala hii kwa utulivu. Huu ni waraka maalumu kwa askari wote wa majeshi yote vikosi vyote Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa lugha ya wazi zaidi nazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa, askari wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM),  askari wa Jeshi la Magereza na wale wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Kuwa mwanajeshi lolote kati ya hayo niliyoyataja si dhambi na si kweli kwamba kuwa mwanajeshi kunakuondolea uwezo wa kufikiri na badala yake ukawa unafikiriwa na watu wengine.

Wala haimaanishi kuwa askari kuwa kama robot ndio nidhamu bora kuliko zote duniani. La hasha! Mimi nilikataa utumwa huo!

Mwaka 1999 nilihitimu elimu ya cheti cha ufundi mchundo, yaani Full Technician Certificate (FTC) katika uhandisi wa Elektroniki na Mawasiliano ya Anga, yaani Electronics & Telecommunications Engineering kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).

Nikiwa bado sijapata kazi ya maana, mwezi Aprili mwaka 2000 niliona tangazo la kazi ya Radio Technician katika Jeshi la Magereza. Nikatuma maombi na kuitwa kwenye usaili uliofanyika Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Magereza Ukonga, Dar es Salaam mwezi Juni 2000.

Wote tuliofaulu usaili tulipangiwa siku ya kuripoti Chuo cha Magereza Kiwira kule Tukuyu, Mbeya.

Kufika kule nilishuhudia mambo ya ajabu. Ingawa wao hufurahia na kusema eti wanakutoa uraiani na kuwa mwanajeshi lakini baadhi ya matendo yanayofanyika wakati wa mafunzo ya jeshi ni ya kuwapumbaza askari wetu ili baadaye wakiwa kazini, watawala wawatumie watakavyo.

Nilishindwa kuvumilia kaulimbiu ya wakufunzi wa jeshi pale walipoelekeza kwamba chochote kruta (askari mpya mafunzoni) unachoambiwa lazima uitikie “ndiyo afande”. Nilishindwa kuitikia kwa mfano pale mkufunzi mmoja mwenye cheo cha koplo alipotutamkia mfululizo wa sentensi zifuatazo:
Mkufunzi: Nyinyi makruta mbona wote hamkuja na majembe?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Hamkuambiwa makao makuu ya jeshi kwamba lazima mje na majembe?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Kwa hiyo kwa kuwa hamkuambiwa na nyinyi hamkuyabeba?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi:  Wote ni wapumbavu pamoja na mama zenu waliowazaa.
Makruta: Ndiyo afande!

Ni hayo pamoja na mambo mengine ya kulazimishwa kwenda kwenye kile kinachoitwa disko, ambapo pamoja na uchovu wa kutwa nzima wa kazi ngumu na nyingi bado ni lazima ukae hapo mpaka saa 4 usiku tena ukinyooshewa kidole tu na mwenzako lazima usimame na kuimbisha wimbo tena kwa tabasamu, wimbo mmoja wapo ukisema “Magereza ninavyokupenda nitakunywa sumu juu yako”, ndiyo yaliyonifanya nikakataa kazi ya jeshi baada ya wiki moja tu ya mafunzo.

Siku niliyokataa jeshi ilikuwa ni Jumatano asubuhi ambapo sikwenda mchakamchaka na wakati wenzako wanatawanyika kufanya usafi wa nje maeneo mbalimbali, mimi nilibeba begi langu na kuanza kuondoka chuoni majira ya saa moja na nusu hivi asubuhi.

Nilikamatwa na mkufunzi mmoja wa jeshi na kupelekwa pamoja na begi langu kwa Ofisa Mafunzo wa chuo. Aliponiuliza sababu nilimtajia mbili, kwanza kwamba sifurahii mambo ya jeshi na kubwa zaidi kwamba mimi ni Msabato na nimeambiwa na wenzangu kwamba hapa hakuna kwenda kusali, siku zote za juma ni kazi.

Kitu ambacho sitaweza maana Sabato takatifu lazima nipumzike! Bila kuuliza zaidi aliconclude kwa kuniambia kwamba, “Sijawahi kuona mtu anaacha kazi kwa ajili ya mambo ya dini.

”Ni dhahiri wewe ulikuja kutupeleleza na hivyo kazi yako imeisha sasa unataka kurudi. Tutakuweka rumande, tena ile ya polisi kwa wiki mbili wakati tunafanya upelelezi juu yako.”

Askari aliyenileta alianza kunivuta ili kunipeleka rumande lakini nilikataa huku nikiendelea kujieleza kwa ofisa mafunzo ili ajue kwamba sikuwa na mpango huo aliousema.

Baada ya kuelemewa na hoja zangu alinipeleka kwa makamu mkuu wa chuo ambaye yeye alitumia zaidi Biblia kunihubiri kwamba nakaidi amri ya mamlaka wakati hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.

Jibu langu lilikuwa fupi na lenye msimamo mzito kwamba ikiwa mamlaka ya wanadamu inafika mahali inanena tofauti na Mungu, Mtume Petro ametuandikia kwamba katika hali ya namna hiyo, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko mwanadamu”.

Na yeye alinishindwa akanipeleka kwa mkuu wa chuo na wao wote wakiwapo. Ushauri waliokuwa wakimpa mkuu wa chuo ni kwamba mimi niwekwe rumande kwanza ili wafanye upelelezi. Lakini sikuyumba katika msimamo wangu.

Nilimweleza  mkuu wa chuo kwamba mimi ni raia  na si mpelelezi. Nilizirudia rudia sababu zangu za kuacha jeshi tena kwa ujasiri mkubwa na kumhakikishia mkuu wa chuo kwamba akinipa hayo ninayoyataka niko tayari kubaki jeshini.
Hatimaye kauli ya mwisho ya mkuu wa chuo ilikuwa ni hii: “Jeshi ni wito. Tunaweza kumlazimisha huyu kijana kuwa mwanajeshi lakini baadaye ikatuletea madhara makubwa sana.” Akamalizia kwa kusema, “chukueni maelezo yake kwa maandishi kisha arudishe vifaa vya jeshi.”

Wakati naondoka nilimsikia ofisa mafunzo akitoa maelekezo kwa walio chini yake kwamba mwanafunzi mwingine wa jeshi akija kuripoti na kwenye daftari akajaza kwamba ni Msabato, msimsajili kwanza mpaka aje kwangu! Sijui kama Wasabato wameendelea kupokewa kwenye hicho chuo cha magereza lakini ninachotaka askari wote wa majeshi yetu yote na vikosi vyote, ni kwamba askari unaweza kusimama kwa miguu yako na kufikiri kwa akili yako mwenyewe!
Ndugu zangu askari, nchi imefika mahali ambapo Waingereza hupenda kupaita ‘critical point’. Ni mahali ambapo wananchi wako tayari kwa mabadiliko na watawala wako tayari kwa mapambano ili kubaki madarakani.

Katika point hii askari wetu wanakuwa na nafasi kubwa ya aidha kuwezesha mabadiliko hayo kutokea kwa wakati wanaoutaka wananchi, tena kwa amani ama kuyachelewesha (si kuyazuia) na kusababisha yatokee baadaye kidogo kuliko wananchi walivyotaka, tena baada ya kumwaga damu nyingi ya Watanzania wasio na hatia!

Napenda kurudia kwamba hakuna jeshi lolote duniani hata kama tungekusanya majeshi yote ya dunia hii na kuyaleta Tanzania hawataweza kuizuia nguvu ya umma pale inapokuwa imeamua kufanya mabadiliko.

Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kile ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya. Tunaweza kusimama imara na kutetea haki za Watanzania tukiwamo na sisi askari.  Niliwahi kugoma kutii amri ya kukamatwa na kuwekwa rumande.
Lakini pia mifano ni mingi na nisingependa kuchukua mifano kutoka nchi za Ulaya kama Uingereza ambako tulishuhudia wananchi wakiandamana mitaani na askari wao hawakuwahi hata kumpiga kofi tu mwandamanaji hata mmoja.
Walipohojiwa na vyombo vya habari walisema dhahiri kwamba waandamanaji ni raia halali  wenye haki ya kufanya kile wanachokifanya kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yao. Katiba ya Tanzania na sheria za nchi hii zinatoa haki kama zile za Uingereza. Tofauti ni utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba na kisheria. Watawala wa Uingereza wako tayari  hata kung’oka madarakani ili kutekeleza matakwa ya nguvu ya umma.

Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung’oa uhai wa raia wengi ili mradi  kuzuia nguvu ya umma inayodai  haki na   wananya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung’oka madarakani, jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia. Na  ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea nyinyi.

Wanaminya haki zenu nyinyi wenyewe, haki za wazazi wenu, dada na ndugu zenu,  marafiki zenu, jamaa zenu na majirani zenu. Chukulia mfano rafiki zangu Mtaki na Edwin. Tumesoma wote shule ya msingi pale Magu.

Nilichaguliwa kujiunga na Mazengo Sekondari, shule kubwa na ya muda  mrefu ambayo sasa imegeuzwa kuwa chuo kikuu bila mabadiliko ya majengo.

Shule iliyokuwa na maabara nne kwa maana ya maabara ya baiolojia, kemia, fizikia na  jiografia. Ilikuwa ni sekondari ya ufundi na hakuna karakana ambayo haikuwapo.

Shule iliyokuwa na walimu wa kutosha, vyumba vya kutosha vya madarasa na vya kulala mabwenini.
Katika bweni la Ujamaa kwa mfano, nilikokuwa naishi mimi, kuna vyumba kadhaa havikuwa na watu. Darasa la Form IVA ambalo nilikuwamo lilikuwa na wanafunzi 21 tu darasani.

Na mazingira mengine mengi ambayo sitaweza kuyataja hapa ambayo yanafanya wanafunzi wa leo wa Chuo Kikuu cha Mt. John wajiulize kama kweli ile ilikuwa ni shule ambayo haina maktaba wala vitabu vya kutosha, na mengineyo mengi mnayoyafahmu.

Nikafaulu kwa kiwango cha daraja la juu lililoniwezesha kuendelea mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri kwenye Umoja wa Mataiifa.

Rafiki zangu nakumbuka mlivyoamua kujiunga na Jeshi la Polisi si kwa sababu mlipenda kazi hiyo ama kwamba mlikuwa na wito wa kuwa polisi kama mnavyodanganywa kwamba jeshi ni wito.

Nakumbuka mlijiunga huku mkilalamika kwamba mnalazimika kujiunga huko kwa sababu kiwango chenu cha ufaulu hakiwapi fursa ya kazi bora zaidi ya hiyo. Lakini mimi nawafahamu vizuri. Najua uwezo wenu wa darasani. Mliathiriwa na mazingira ya hovyo ya shule mlizosoma.

Rafiki zangu nyinyi wote leo ni wakuu wa vituo vikuu vya polisi vya wilaya katika wilaya za Mbozi na Igunga.
Leo hii mimi nimeacha kazi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kushiriki vema katika mapambano ya kutafuta ukombozi wa taifa hili.

Wadogo zenu na wadogo zangu mnawajua wako katika juhudi za kutafuta maisha lakini ni magumu. Wengine walikosa kabisa nafasi ya kujiunga hata na hiyo Magu Day.

Wakaishia Bulima na Kinango, ambako hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakafeli kabisa na leo wanahangaika hapa na pale lakini watawala wanawawekea mazingira magumu mno ya kuendesha maisha.

Na sasa chukulia nao wametambua hali yao duni inasababishwa na watawala walafi na walaghai. Wamejaribu kutumia njia za kidiplomasia kudai haki zao wanakutana na watu wanaitwa wakuu wa wilaya na mikoa.

Wanaamua kuandamana, mnashiriki kuamrisha askari walio chini yenu kuwapiga na kuwaweka rumande na hatimaye kuwafungulia kesi za kubumba!

Askari wetu igeni mfano wa askari wa Misri! Pale wananchi walipoamua kuandamana kukomesha utawala wa kidhalimu wa miaka 30 chini ya  Hosni Mubarak, askari waliwalinda badala ya kuwapiga.

Walikataa kwa sababu hata wao walikuwa wakiumizwa na Mubarak lakini zaidi ya hayo, waliokuwa wakiandamana walikuwa ni dada zao na ndugu zao na marafiki zao.

Hivi sasa nchi iko njia panda. Ugumu wa maisha umeongezeka mara nne na zaidi. Watawala hawalioni hilo wala hawajishughulishi kurekebisha hali ya mambo hususan hali ya uchumi.

Wako busy na kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Mawaziri wako busy na kampeni za kuteuliwa kuwa wagombea wa urais kupitia chama tawala hapo 2015 na rais naye yuko busy kuandaa mtu wake ambaye anadhani akimrithisha jumba jeupe la pale Magogoni atasema mwacheni Ndugu Kikwete apumzike kwa amani.

Taifa limeamua kuandika katiba mpya, rais na serikali yake na chama chake wameamua kuuteka mchakato ingawa haikuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi ili tu waturudishie katiba ya mwaka 1977 na kuipa jina juu ya jalada KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2014.

Natambua juhudi zinazoendelea hasa zikiongozwa na CHADEMA kujaribu kumkumbusha rais kwamba katiba iko juu yake na katiba ni mali ya wananchi na yeye anaajiriwa kwa katiba hiyo na si yeye kujiandalia katiba ili atawale kwa ulaini.

Lakini juhudi za kidiplomasia zikishindikana hapo ndipo itabidi haki ya watu idaiwe kwa maandamano na hapo askari wote tuungane na kuwa kama Misri, kwa kuwa Katiba mpya ni kwa masilahi yenu pia! Jaribuni kutafakari!
             ****MWISHO***


KUHOJIWA KIBANDA: TAARIFA YA JUKWAA LA WAHARIRI


UTANGULIZI

1. Ijumaa iliyopita, Mhariri Mtendaji wa Free Media Ltd, wazalishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Absalom Kibanda alishikiliwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini.

2. Kiini cha tukio hili ni makala iliyochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima Jumatano, Novemba 30, 2011 ikiwa na kichwa kisemacho "Waraka maalum kwa askari wote".

3. Mwandishi wa makala hiyo, Samson Mwigamba ambaye tayari amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi analalamikia hulka ya polisi wa chini kutii amri hata kama amri hizo zina madhara kwa nchi na kwa mtizamo wake anasema hali hiyo inaweza kuifikisha nchi pabaya siku zijazo.

UTENDAJI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI

4. Umekuwa ni utamaduni kwa Msajili wa Magazeti ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) kuchukua hatua za kuvibana vyombo vya habari, hususan magazeti ambayo yamekuwa yakionekana kukiuka sheria za nchi katika uandishi wake.

5. Chini ya utaratibu huu ambao hata hivyo umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa habari, Maelezo humwandikia barua Mhariri husika kuhusu kosa linalodaiwa kufanywa katika gazeti lake, na kutaka atoe maelezo au afike katika ofisi hizo kwa ajili ya kuhojiwa.

6. Kupitia Maelezo, hatua mbalimbali zimechukuliwa na pande husika ikiwa ni pamoja na magazeti kupewa barua za onyo, kupewa fursa ya kusahihisha taarifa husika na katika matukio machache yasiyopendeza baadhi yamewahi kufungiwa na mengine kufutwa kabisa.

7. Licha ya kasoro zake, jambo la msingi ni kwamba utaratibu wa Msajili wa Magazeti walau umekuwa ukitoa fursa watendaji wa magazeti yanayolalamikiwa kutoa maelezo ya upande wa pili lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba Uhuru wa Habari hauminywi kiasi cha kuukosesha umma taarifa muhimu za nchi na mambo yanayofanyika nchini.

KUKAMATWA KWA KIBANDA

Jukwaa la Wahariri limefuatilia kwa karibu sana tangu kukamatwa kwa Kibanda na mtindo uliotumiwa na Polisi katika kushughulikia suala hilo na kubaini yafuatayo:

8. Kwanza Makala ambayo ni chimbuko la kukamatwa kwa Mwigamba na baadaye Kibanda haikuwahi kulalamikiwa na Ofisi ya Msajili wa Magazeti kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa taarifa nyingine nyingi, si kwa gazeti la Tanzania Daima tu, bali hata kwa magazeti mengine.

9. Kwa maana hiyo hakuna barua yoyote kutoka Maelezo ambayo iliwasilishwa Tanzania Daima ikimtaka Mhariri Mtendaji kutoa maelezo ya kimaandishi au kufika kwa msajili kujibu tuhuma za ukiukwaji wa maadili ama sheria katika makala hiyo ya Novemba 30, 2011.

10. Hakuna taarifa zozote za mtiririko wa kimatukio katika Idara ya Habari (Maelezo) au kwingineko Serikalini ambazo zinabainisha iwapo kulikuwa na onyo lolote kwa Tanzania Daima kuhusu mwenendo wake au kuhusu makala za Samson Mwigamba.

MTIZAMO NA MSIMAMO WA TEF

11. Kutokana na hali hiyo, TEF inaona kwamba kuna msukumo usio wa kawaida nyuma ya hatua ya Polisi ya kumhoji Kibanda na kwamba mwelekeo ni kuminya uhuru wa Habari na Uhuru wa kujieleza ambao umetolwa chini ya misingi ya Katiba ya nchi.

12. Msukumo huu unatokana na kuibuka ghafla kwa vyombo vya dola na zamu hii Polisi wakitumia muda mrefu katika kile walichokiita kuwa ni uchochezi, hivyo kuwafungulia wahusika KESI ZA JINAI.

13. Mashtaka haya dhidi ya Kibada na Mwigamba yanatushawishi kuamini taarifa zisizo rasmi juu ya kuwapo kwa mpango wa kuwashughulikia baadhi ya Wahariri na Waandishi wa Habari ambao wamekuwa msitari wa mbele kukosoa waziwazi miendendo ya watawala.

14. Sisi tunasema hali hii haikubaliki kwani inalenga kurejesha demokrasia ya Taifa hili nyuma zaidi ya miaka 50 iliyopita, kwa kuminya uhuru wa kujieleza na haki ya kutoa na kupata habari.

15. Mwenendo wa aina hii wa kuamu kuwashati wahariri kwa makosa ya jinai ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu, hasa pale vyombo vya dola vinapotumika kwa mtindo ambao umetumiwa kuwashughulikia Kibada na Mwigamba.

16. Ikumbukwe kwamba dhamira ya kupambana na wakosoaji wa utendaji Serikalini siyo tu kwamba inaathiri dhana nzima ya utawala bora wa nchi, bali inaliweka Taifa katika hatari ya kutumbukia katika uovu uliokithiri hasa pale wenye dhamana watakapofanya wapendavyo kwa kuwa tu vyombo vya habari vitakuwa vibezibwa midomo.

17. Kwa kuwa hii inaonekana kuwa dhamira rasmi ya Serikali kutumia dola kudhibiti uhuru wa habari, tunatoa mwito kwa watawala wetu kutafakari upya na ikiwezekana kuachana kabisa na dhamira hiyo.

NEVILLE MEENA,
KATIBU MKUU – TEF
KWA NIABA YA BODI YA JUKWAA LA WAHARIRI

MAGAZETI YA AFRKA YAPOTOSHWA KUHUSU HABARI ZA MIKE TYSON KUBADILISHWA KUWA MWANAMKE



Tarehe 12/12/2012   iligeuka kuwa siku ya wajinga duniani badala ya April Mosi baada ya magazeti mengi ya Afrika na hasa Tanzania kuingizwa mkenge na habari ya kubuni ya Mike Tyson kubadilisha jinsia na kuwa mwanamke.

Bahati mbaya sana ni kuwa bado watanzania wengi yakiwemo magazeti na hata baadhi ya vituo vya radio vimeendelea kuisema habari hiyo ya kupotosha kama vile ni ya kweli.


Habari hiyo hata hivyo iliandikwa mwishoni mwa mwezi November na website ya nchini Uingereza ambayo huandika habari za kubuni iitwayo NewsBiscuit.

Magazeti maarufu nchini yakiwemo Mwananchi na Jambo Leo yaliiandika habari hiyo pamoja na magazeti mengine makubwa barani Afrika kama The Standard la Zimbabwe na website ya Ghana SpyGhana.

Kwa mujibu wa BBC,NewsBiscuit ilidaiwa kuelemewa zaidi jana kutokana na wasomaji kuwa wengi kutoka Afrika.

“Tumepata wasomaji zaidi ya nusu kutoka Afrika katika siku chache zilizopita ambao tungetegemea kuwapata kwa mwezi mzima,” mwandishi wa mtandao huo John O’Farrell aliiambia BBC.

Alisema habari hiyo ilisomwa zaidi ya mara 50,000 katika siku chache tu ikiwa ni mara 20 zaidi ya kawaida.


MISA -TAN WAPINGA KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MWANAHALISI


TAARIFA KWA UMMA
Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania MISA-Tanzania) inasikitika kuarifu umma wa watanzania kwamba inapinga vikali kitendo cha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Msajili wa Magazeti Tanzania Bara kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi kuanzia tarehe 30 Julai 2012. 

Katika taarifa iliyotolewa na serikali kupitia tangazo lake lililochapishwa kwenye magazeti mbalimbali hapa nchini na kunukuu kutolewa kwa amri hiyo kupitia gazeti la serikali (Government Notice)toleo namba 258 la tarehe 27 Julai 2012, serikali imeeleza kama ifuatavyo:

“Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi kwa mujibu wa sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu namba 25 (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai 2012”

Aidha, tamko hilo la serikali limeeleza pia kuwa sababu za msingi za kulifungia gazeti hilo ni kufuatia machapisho mbalimbali ya gazeti hilo kwenye toleo Na. 302, Na. 303 pamoja na toleo Na. 304 yote yakiwa ya mwezi Julai 2012 pamoja na machapisho mengine yaliyotangulia. Serikali imeeleza kuwa machapisho hayo yamekuwa “yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii”
 
Hata hivyo, serikali haikubainisha ni habari zipi katika machapisho hayo ambazo zinaeneza na kujenga hofu kwa jamii. Kitendo hicho cha kutobainisha habari husika kinatufanya sisi kama wanahabari na watetezi wa haki ya kupata taarifa pamoja na uhuru wa vyombo vya habari nchini na katika kanda ya kusini mwa Afrika kutoridhia maamuzi ya serikali kwani yamehusisha masuala ambayo hayakuwekwa bayana.

Ni kwa mashaka makubwa ambayo yanatokana na tamko husika la serikali kwa kutumia maneno yafuatayo:

“Kuanzia sasa serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa makusudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu”
 
MISA–Tanzania inasikitishwa na kauli hiyo kwani kauli hiyo ni kudhihirisha matumizi mabaya ya sheria zilizopo katika kukandamiza uhuru wa kupata taarifa na uhuru wa vyombo vya habari kinyume na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 (b) na (d) kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005.

Haki ya kutafuta, kupata na kutoa taarifa ni haki ya msingi ya kila binadamu na imetambuliwa hivyo na Katiba ya Tanzania. Haki hii imetambuliwa pia na mikataba mbalimbali ya Kimataifa ambayo Tanzania imeiridhia bila masharti yoyote.

Kama kweli kuna taarifa za uchochezi zilizochapishwa na gazeti la MwanaHalisi na kuhatarisha amani na utulivu wa nchi, ni vyema serikali ingebainisha taarifa hizo kwenye chapisho husika na siyo kuorodhesha machapisho mbalimbali kama sababu yake ya kulifungia gazeti.

Hata hivyo, mamlaka ya serikali kufungia gazeti kupitia msajili wa magazeti ni ukiukwaji wa misingi ya haki za binadamu na matumizi makubwa ya madaraka.

Ni kwa sababu hizo kwamba Ripoti ya Haki za Binadamu iliyowahi kuandaliwa na kutolewa na Tume maalumu iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujulikana kama Tume ya Jaji Nyalali mwaka 1992 ilibainisha sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 kuwa ni miongoni mwa sheria arobaini ambazo zinakandamiza haki za binadamu nchini. Sheria hiyo haina budi kufutwa kwenye vitabu vya sheria za nchi hii.

Kitendo cha kulifungia gazeti la MwanaHalisi kwa muda usiojulikana kinaweza kusababisha hofu kubwa kwa watetezi wa haki za binadamu na wanahabari kwa ujumla. Kitendo hicho kinafuatia kile cha kuwakamata na kuwaweka rumande (Oysterbay Polisi) wanaharakati zaidi ya kumi kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo kuandamana kufuatia mgomo wa Madaktari mnamo tarehe 9 mwezi Februari 2012. 

MISA –Tanzania inalaani vikali matumizi mabaya ya Dola katika kunyamazisha wanahabari wanapojaribu na kuthubutu kufuatilia matukio mbalimbali na kuarifu umma kuhusu yale waliyoyafanyia kazi kwa kina. Ni rai yetu kwa serikali kuwa ni vyema wabainishe taarifa mahsusi zilizopelekea maamuzi ya kufungia gazeti la MwanaHalisi ili kutuondolea hofu sisi tunaotetea haki na uhuru wa vyombo vya habari. Kuendelea kuficha taarifa husika ni kuendelea kuikanyaga Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (ibara ya 18) kupitia kivuli cha Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo kimsingi imepitwa na wakati na haiwezi kutumika kinyume na Katiba ya nchi. 

Ni rai yetu pia kwa serikali ya Tanzania kwamba izingatie Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika yale yenye kuhamasisha utoaji haki kuliko kujikita kwenye kifungu cha 30 cha Katiba hiyo ambacho kimsingi kinaweka mipaka maalumu ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Mipaka hiyo haionekani kuzingatiwa na serikali katika kulifungia gazeti la MwanaHalisi.
 
Kwa taarifa hii kwa umma, tunaiomba pia serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulifungulia gazeti la MwanaHalisi mapema iwezekanavyo na bila masharti ili kuwawezesha watanzania kuendelea kunufaika na taarifa zinazochapishwa na gazeti hilo ilmradi maadili ya uandishi wa habari yazingatiwe. Hii ni haki ya msingi kwa kila mtu na ni vyema aione ikitekelezeka.

Taarifa hii imetolewa na kusaini hapa Dar es salaam leo tarehe 31 Julai 2012.
Mohammed Tibanyendera
Mwenyekiti, MISA-TAN

AKABIZU OFFICIAL VIDEO


BABY CANDY, SKAINA NA JACK CHUZ WAGOMBEA PENZI LA TIMBULO....


MASTAA wasichana wa mjini, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz, Skyner Ally ‘Skaina’ na Baby Candy wamejikuta wakirushiana matusi kupitia mtandao wa kijamii wa BBM kisa kikiwa ni msanii wa Bongo Fleva, Ally Timbulo. 

Katika sakata hilo, Jack Chuz alitajwa kuwa ndiye chanzo cha mabinti hao kugombana kwani mmoja alikuwa akimtetea shoga yake kwa kudai anataka kunyang’anywa bwana.

Aliyelianzisha bifu hilo ni msanii mmoja rafiki yao na akina Baby Candy ambaye alianza kwa kumtumia ujumbe wa matusi Skaina na kumwambia anaiba mabwana wa wenzake akimaanisha anataka kumuiba Timbulo.


Baada ya matusi kutua kwa Skaina aliyetuma ‘pini’ ya Timbulo mtandaoni akimuombea marafiki, Baby Candy naye aliamua kumtupia Skaina maneno makali akimalizia kwa kumwambia kuwa anaingilia vitu asivyovijua.


Ilifahamika kuwa baada ya kusoma ujumbe wa Baby Candy, Skaina alimporomoshea matusi mazito ambayo hayaandikiki akimalizia kwa kumwambia kuwa hana lolote bali anatafuta tu ustaa mtandaoni.




Hata hivyo, inaelezwa kuwa matusi hayo yalimkera Timbulo ambaye naye alijibu kupitia BBM akidai kuwa asingependa jina lake litumike vibaya kwani hana demu wala hawara kati yao hivyo anawaona kama machangu tu.

SAKATA LA NAIBU WAZIRI WA ELIMU KUWA NA ELIMU FEKI PAMOJA NA JINA FEKI LACHUKUA SURA MPYA.....!!!


NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, amesema yupo tayari kumthibitishia Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Joseph Mbilinyi, maarufu 'Sugu', juu ya elimu aliyonayo kama alivyodai mbunge huyo.

Bw. Mulugo aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na Majira kuhusu madai ya Bw. Mbilinyi ambayo ameyatoa katika vyombo vya habari kuwa, Waziri huyo ana elimu ya kuunga unga na jina lake kamili ni Amim.

Alisema kauli ya Bw. Mbilinyi haina ukweli wowote bali yeye ni msomi na yupo tayari kuthibitisha ukweli huo kwa umma.

“Mimi na Bw. Mbilinyi tuna vilema vingi, akitaka tuumbuane yatabainika mengi hasa katika upande wake, namfahamu muda  mrefu kwa sababu nimesoma naye shule moja, nafahamu mambo yake mengi lakini kutokana na hekima zangu sihitaji malumbano na yeye,” alisema Bw. Mulugo.

Alidai kumshangaa Bw. Mbilinyi, kuzungumzia jambo ambalo halifahamu lakini kwa kumsaidia ili asielendelee kuonekana mwanasiasa muongo, aitishe mkutano na waandishi wa habari na yeye atakuwa tayari kuthibitisha elimu yake kwa umma.

Bw. Mulugo aliongeza kuwa, ni kweli wakati anasoma alikuwa akitumia jina la Amim na baada ya kufika elimu ya juu alianza kutumia jina la Philipo ambalo ni la ukoo ambapo Bw. Mbilinyi kama angekuwa makini, angefuatilia kwenye ukoo wake ili kujua jina hilo linamuhusu au la.

Aliongeza kuwa, dhamira yake ni kuhakikisha kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ambalo hivi sasa linashikiliwa na Bw. Mbilinyi, mwaka 2015 linarudi CCM na ukweli huo utathibitika katika uchaguzi.

Mimi ni Waziri kutoka CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu NEC, hivyo Bw. Mbilinyi, asifikiri kuzua maneno hayo yatanitisha hadi nishindwe kutekeleza sera za chama changu,” alisema.

Alisema ibara ya 5 ya Katiba ya CCM, inamwongoza kuhakikisha chama chake kinashinda uchaguzi wa dola wa ngazi zote pamoja na kulirudisha jimbo la Mbeya Mjini kutoka upinzani.

“Katika Uchaguzi Mkuu ujao, nitatumia nguvu zote kuhakikisha jimbo la Mbeya Mjini linarudi CCM, ninachoweza kumshauri Bw. Mbilinyi,  ajifunze kutokana na makosa kwani ameanza kunitafuta siku nyingi lakini mimi sikuwa na muda wa kumjibu bali niliendelea kutekeleza majukumu niliyonayo,” alisema.

Alisema Mbunge huyo na chama chake walijibiwa na wananchi wa Saza katika mkutano wa CHADEMA uliofanyika katika Wilaya ya Chunya na kusahau kilichowapeleka ni kampeni hatimaye wakaanza kunadi elimu ya Mulugo badala yake waliambulia kufukuzwa.

Aliongeza kuwa, Bw. Mbilinyi alipaswa kulisema na hilo kama walifukuzwa na wananchi wa Saza ambao walimwambia wao, wanamfahamu viziri Bw. Mulugo na wamemsomesha wenyewe kwa pesa zao baada ya kuthibitika ni yatima.

Alisema wananchi hao walidai kuchoshwa na matusi ya Bw. Mbilinyi dhidi yake na kumtungia uongo lakini yeye hana
muda wa kulumbana naye bali atamjibu kwa ushahidi.

Kauli ya Bw. Mulugo imekuja siku chache baada ya Bw. Mbilinyi kudai kuwa, elimu ya Waziri huyo ni ya kuunga unga kwani alisoma naye Sekondari ya Mbeya Day, wakati huo akiitwa Amim si Philipo Mulugo hivyo kuanzia sasa ataendelea kumuita jina lake halisi na kusisitiza hana uwezo wa kumng'oa jimboni kwake. 


UGOMVI ULIANZIA KWENYE HII HOTUBA 

AIBU: TABIA YA KUPIGA PICHA ZA UTUPU YAENDELEA KUWATAFUNA AKINA DADA...!

Written By Mike Ntobi on Sunday, December 30, 2012 | 12:40 PM


AIBU.....AIBU.......

Tabia  ya  kupiga picha  chafu  za utupu  imeendela kuwatafuna  akina  dada  hapa  nchini.....

Tabia hii  ilianzia  kwa  wasanii maarufu kama  WEMA SEPETU,  JACK  WA  CHUZ,  LULU MICHAEL  RAYUU na sasa  imeingia  kwa  warembo wa  kawaida ......





Pamoja na jitihada za kuwaanika watu  hawa, tabia hii  imeendelea kuota mizizi kila kukicha.Wahusika wakuu wa  uchafu  huu ni akina dada.......

Iko haja kwa  akina  dada  kujitathmini.....Kwa  nini  kila siku ni wao tu???  Kwa nini  ukubali  kupigwa  ukiwa  mtupu  tena  na  mtu ambaye  mmekutana  na kupeana  penzi tu????....



Pengine ni  tamaa ya pesa.Nadhani hii ni biashara.Nashawishika  kuamini kuwa hawa  watu hupiga hizi picha kwa makubaliano maalum ya fungu flani la pesa.....



Nasema hivi maana  ni ngumu sana kwa mtu mwenye  akili zake  kukubali  kuaibika kisa  PENZI.

Na kama  ni tamaa  ya pesa, basi  haya  ndo matunda yake  maana  KILA  MTU HUVUNA  APANDALO.... 
--------------------------------------------------------------
NB:

Kuna  baadhi  ya  watu  wanalaum  kwamba hatujatenda  haki.Kabla  ya kulaumu jiulize yafuatayo:

1.Wasanii  wakikosea kila kitu huwekwa  hadharani  na hao  hao wanaolaum hushangilia.

2. Jiulize picha zimesambaa vipi?   wao ndo  waliozisambaza kwa sababu wakati  wa  starehe zao  walikuwa wawili tu chumbani.

3.Wema Sepetu akijiachia  wote  humponda kwa  kila aina  ya  tusi au neno baya.Tuache ushabiki.Haya  mambo hayafai

UOZO WA NORA WAANIKWA NA MUME WAKE.....!



MUME wa mcheza filamu mahiri za Kibongo Nuru Nassoro ‘Nora’, Masoud Ally ‘Luqman’ ameamua kuvunja ukimya baada mkewe huyo kueleza sababu zilizofanya ndoa yao kuvunjika ambazo anadai siyo za kweli. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Luqman ambaye alitumia zaidi ya saa mbili kutoa ufafanuzi kuhusiana na  habari hiyo, alikanusha vikali kuwa wazazi wake ndiyo chanzo cha kufanya ndoa yao ivunjike.

Alisema kuwa mama yake alikuwa akimpenda sana Nora mpaka staa huyo alikiri kuwa mkwewe huyo anampenda, sasa anaumia kumsikia akidai ndoa yake ilivunjwa na wazazi wake.



Luqman alizidi kutiririka kuwa katika maisha yake ya ndoa aliyoishi na Nora, amewahi kuwa na furaha mara mbili tu kutokana na ugomvi wa kila siku ambao mara nyingi ulikuwa ukisababishwa na Nora.

“Kiukweli ndoa yangu nakumbuka imewahi kuwa na furaha mara mbili tu lakini kipindi chote ilikuwa ni ugomvi usioisha,” alisema.


Aliendelea kusema kuwa kutokana na ugomvi wa kila siku,  kuna siku Nora alishika kiwembe na kumchana nacho mkononi, hali iliyosababisha ashonwe nyuzi tano.

Alisema kuwa alikuwa akijitahidi kujishusha ili kuinusuru ndoa yake kwa sababu bado alikuwa akimpenda sana mke wake huyo lakini hakufanikiwa na kwamba siku nyingine Nora alimshikia kisu kisa kikiwa ni meseji ambayo hakuituma yeye.


Aliendelea kuweka wazi kuwa kutokana na migogoro ya hapa na pale, alishampa talaka zaidi ya mara mbili na kumrudia tena akidhani labda atajirekebisha na kuwa sawa lakini haikuwa hivyo.



“Hii talaka ya mwisho niliyotoa ilikuwa ni ya tatu  lakini yote hayo ni kwa sababu nilimpenda sana mke wangu,”alisema na kuongeza kuwa waliamua kuhamia Zanzibar ambapo Nora mwenyewe alikupenda.

Hata hivyo, walipofika huko bado aliendelea kumsumbua na alijaribu kumtishia kuwa kama ataendelea hivyo ataoa mke mwingine ambapo kauli hiyo ilimkera Nora na kuamua kurudi Dar.


Alisema aliporudi Dar, mara kwa mara alikuwa akimsihi arudi wakaendelee kuishi lakini Nora alikuwa akikataa na ndipo alipoamua kuoa mwanamke mwingine ambaye kwa hivi sasa tayari wamezaa naye mtoto mmoja.


“Nilikuwa nikijaribu sana kumbembeleza Nora arudi ili tuendelee kuishi lakini hakuwa tayari ndipo nilipoamua kuoa mke mwingine,” alimalizia Luqman.

IRENE UWOYA ASHAREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUTOA MISAADA MBALIMBALI



Tofauti na mastaa wengine ambao huangusha party ya nguvu kusherehekea siku zao za kuzaliwa, hivi karibuni Irene Uwoya aliamua kufanya kitu tofauti katika siku yake ya kuzaliwa, December 18.

Muigizaji huyo mrembo aliamua kwenda kwenye hospitali ya Mwananyamala kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa.

irene 4
irene 3
irene 2
irene 1

"NAJUTA KUTEMBEA NA MUME WA MTU"....TIKO



MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tiko Hassan ‘Tiko’ amefunguka kuwa anajuta kutembea na mume wa mtu kwani majirani wanamuandama kwa maneno. 

Akizungumza na suala  hilo  juzikati jijini Dar, Tiko alisema kutokana na kuandamwa na maneno juu ya tabia hiyo ya kutembea na mume wa mtu  ameamua kutafuta mwanaume ambaye yupo singo.

“! Najuta mwenzangu. Bora nitafute mwanaume ambaye yupo singo waache kunisemasema kila siku,” alisema Tiko.

MZEE MAJUTO AJIPANGA KUTOKA NA "PATASHIKA" AMBAYO NI ZAIDI YA KOMEDI




MCHEKESHAJI mkongwe, Amri Athuman ‘King Majuto’ hivi karibuni ataanza kuonekana kwenye kazi mpya iitwayo “Patashika”


Katika kazi hiyo iliyojaa vichekesho vya kuvunja mbavu, Majuto atacheza kama baba wa familia mwenye vibweka vingi vya kustaajabisha, vinavyowaacha watu hoi kila siku mtaani kwao.

“Nategemea kufanya kitu cha tofauti ili mashabiki waweze kujua mimi ninaweza kuigiza ndiyo maana ninaigiza kama baba wa vibweka kwahiyo wadau wangu wategemee vimbwenga vya kustajabisha” alisema gwiji huyo wakuchekesha.

Mbali ya Majuto katika picha hiyo pia inawashirikisha nyota wengine ambao ni wakonnge kwenye Nyanja za uchekeshaji wakiwemo Pembe, Senga, Kingwendu, Full Tank na Difenda.

Kazi hiyo imepangwa kuingia sokoni hivi karibuni, ambako itapatikana mikoa yote hapa nchini, kwenye VCD pamoja na DVD.

"SIPO TAYARI KUZALISHWA KWA SASA"...BABY MADAHA



STAA wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha amefunguka kuwa hayupo tayari kuzaa kwa sasa.

Akizungumza kwa kujiamini, Baby Madaha aliweka wazi kuwa yupo bize sana na kazi zake za muziki na filamu hivyo suala la kunyonyesha litampotezea muda wake.

“We ubebe mimba sasa hivi, uilee halafu uje kunyonyesha, haya madili ya mjini yote yatafanywa na nani?” alihoji Baby Madaha na kuongeza:

“Mikakati yangu kwa mwaka 2013 ni kuhakikisha nafanya mapinduzi makubwa katika muziki wa Bongo Fleva na filamu.”

"NAWAPENDA MARAFIKI WA KIUME MAANA HAWANA MAJUNGU KAMA WANAWAKE".....QUEEN DARLEEN



STAA anayefanya poa na ngoma ‘Kokoro’, Queen Darleen, ameuambia mtandao huu  kuwa anajisikia raha kuwa na marafiki wengi wa kiume kuliko wanawake, huku akiamini kuwa tabia za baadhi ya wanawake ndizo zinazomfanya awe hivyo.

Msanii huyo ni mmoja ya wanawake wenye staili za kipekee kabisa kwenye game ingawa ndani ya mwaka huu amekuja kivingine kabisa baada ya kuwa kimya kwa muda na kuteka mashabiki kupitia kibao cha ‘Maneno Maneno’.

Kauli ya msanii huyo imekuja baada ya kuzungumza na mwandishi wetu alietaka kujua ni kundi gani la watu ambao hupenda kuwa nao karibu sana na kubandilishana mawazo ndipo yenye maana, ndipo alipofunguka kuwa mara nyingi huwa karibu na wanaume na si wanawake.

Alisema kuwa karibu na wanaume haimanishi kwamba ni mabwana zake hapana bali anaona ni watu ambao anaendana nao ingawa tabia zake si za kiume kama baadhi ya watu wanavyopenda kudhani kutoka na staili zake au aina ya kazi anazofanya.

“Kuna watu wanajua mimi nina tabia za kiume hiyo inawezekana kwa sababu wao ndo wanaosema, napenda sana kuwa na watu ambao tutafanya mambo ya maendeleo na si kuzungumza mapenzi na upuuzi muda wote hiyo ndo sababu kubwa inayonifanya nijiweke sana kwa wanaume,”alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa anahisi akijiweka karibu sana na wanawake hakuna kitu kikubwa watakachokuwa wanazungumza zaidi ya majungu na mapenzi, ingawa hata wanaume baadhi yao wako hivyo ila si kama wanawake ambao hupoteza mda mwingi kujadili ujinga.

“SCENES ZA MAPENZI KWENYE FILAMU ZINAWAUMBUA WASANII WANAONUKA MIDOMO” – IRENE UWOYA



MSANII wa filamu anayejichukulia umaarufu bongo Irene Uwoyaamedai kuwa kuna baadhi ya wasanii wenye majina makubwa wanapenda kucheza filamu za mapenzi na uchezeana huku wakishindwa kuelewa kuwa wananuka midono na mara nyingine huwa wanavumulia pasipo kutoa ukweli huo.

Kauli kama ya msanii huyu iliwahi kutolewa na Janet Jackson kwenye filamu ya ‘Poetic Justice’ iliyozinduliwa mwaka 1993 akimtaka Tupac Shakur kupima vizuri vya ukimwi kwani kuna kipande walitakiwa kuonekana wakipeana midomo kwani walicheza kama wapenzi ndani ya filamu hiyo, ndiyo kitu ambacho hata kwa wasanii wa kitanzania wanatakiwa kujifunza na si kukurupuka kupeana midomo..

Uwoya alisema kuwa kuna sehemu huwa wanakosea na kupeana midomo bila kupima afya kwani wapo wasanii wengine si wasafi na wananuka midomo huku wengine wakiwa wanatumia sana dawa za kulevya hivyo kuna hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa endapo wasipo chukua hatua.

Alisema kuwa wengine wanajijua walivyo lakini wanashindwa kujisafisha na kuwa katika hali nzuri badala yake ndani ya filamu wanaanza kupeanda kiss na kuchezeana bila kujua afya ziko vipi.

“Sasaivi naanza kuwa mkali kwa sababu endapo tukiendelea kuwa kimya tunaweza kujikuta magonjwa yanatukuta hivi hivi” aliongeza.

Hata hivyo msanii huyo aliwashauri baadhi ya wasanii wenye tabia za kupenda kupeana midomo ndani ya filamu wawe makini kwani huwezi jua ni ugonjwa gani anaoweza kupata, na kikubwa zaidi ni kupima kabla ya kazi kuanza ili kama kuna mtu mwenye tatizo apewe tiba mapema.

KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE HAKUFAI......EPUKA KUJIZIBA MATAMBARA MAANA NI AIBU....!!!!!



Hii  ni picha  ya  mashoga ambao  bado  hawajitambui......Ni  jamii fulani  ya  watu  ambao UZUNGU  umewaponza.....

Ndugu  zangu,  ni  imani yetu  kuwa  jamii yetu  inahitaji kuelimishwa  sana ili tuweze  kuikomboa  mikononi mwa  hii  dhambi ambayo  ndo  dhambi kubwa  kuliko  zote......

 Tusipende  kuiga  kila kitu toka  kwa  WEUPE.Kabla  hujafanya maamuzi  yoyote Ni bora ukumbuke mambo yafuatayo:-
 
1. TIGO  Sio tendo asilia katika swala zima la ngono na mapenzi hivyo kumbuka unapoamua kugawa tako kuwa na uhakika ndio kitu unataka kukifanya na sio kukifanya kwa vile “mchumba” kaomba/anataka…..

Wewe ndio mwenye maamuzi makuu ya nini unataka kifanyike mwilini mwako. ........

  2.Mpaka  sasa  sidhani  kama  kuna kondom  imara yenye uwezo wakustahimili joto la huko "nyuma" .....

Kondom za kawaida  husababisha muwasho utakaoweza kukusababishia maambukizo mengine yatokanayo na wadudu asilia walioko sehemu hiyo ya haja  kubwa......

 3.Mara mishipa ya makalioni  ikitanuka kutokana na kufanywa huko mara kwa mara huwa haijirudi kama ilivyo kwenye uke kwa vile haikuumbwa kwa ajili ya shughuli hiyo.

EPUKA  KUJIZIBA  MATAMBARA....UTU  WAKO NI  BORA  KULIKO  HIYO  STAREHE  YA  DAKIKA CHACHE 

RIHANNA AJIACHIA TENA AKIWA MTUPU......



Picha za Mwanadada asiyeishiwa  vituko ( RIHANNA)  zimeendelea kusambaa kwa  kasi  katika  mitandao mbali mbali ya udaku.....

Picha hizo  zinazomuonesha  RIHANNA  akiwa mtupu  zilianza  kusambaa  kwa kasi jana mchana  na mpaka  sasa msanii  huyo  hajatoa kauli  yoyote kuhusiana  na picha  hizo.




Get our toolbar!Get our toolbar!
  • Alexaporn - XXX (+18) Search!Alexaporn - XXX (+18) Search!
 
Sell Your Products At TripleClicks!Share Links Earn Money!
cafepress.com/nicemike
Sale Online!
Support : MIKENTOBI | Creating Website | Johny Template | Mas Template | UviOo | SFI

Copyright © 2010 - 2014. MIKENTOBI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Modified and Published by MIKENTOBI
Proudly powered by Blogger